Uchimbaji wa msingi wa jengo la utawala ukiwa umekamilika
Halmshauri ya Wilaya ya Mbulu imeanza kutekeleza shughuli za Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya itakayogharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 1.5 unaoendelea katika mji mdogo wa Dongobesh tangu mwezi januari kwa hatua za awali kama vile uchimbaji wa msingi kwa majengo yote saba ya Utawala,Wagonjwa wa nje,Maabara,Wodi ya Wazazi,Stoo ya Madawa, na Mionzi yatakayopatikana katika Hospitali hiyo,huku ujenzi huo ukitarajiwa kukamilika Juni Mwaka 2019.
upokeaji wa simenti kwa ajili ya ujenzi ukiendelea toka kampuni ya Dangote na kuhifadhiwa kwenye banda maalum lakuhifadhi vifaa
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Wananchi wa Kata za Dongobesh, Dinamu,Bashay,Tumati na maeneo mbalimbali ndani ya Wilaya ya Mbulu wameishukuru Serikali ya Awamu ya tano chini ya Rais Dokta John Pombe Magufuli kwa kuendelea kuimarisha Sekta ya Afya na kwa kuendelea kuimarisha miradi mbalimbali ya maendeleo katika makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu. Hivyo Ujenzi wa Hospitali hiyo utakuwa Mkombozi wa Afya zao kwani huduma itasogezwa karibu.
ujenzi wa choo na bafu cha muda kitachotumika kikiwa kimekamilika tayari kwa matumizi
Wanananchi hao wameendelea kuishukuru Serikali kwa kukubali kuleta Fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali hiyo ambapo itawapunguzia gharama ya upatikanaji wa baadhi ya huduma walizokuwa wakizikosa kwa vituo vya afya na zahanati zilizopo katika kata zao,ambapo mara nyingi Wananchi hao wamekuwa wakilazimika kufuata huduma hizo Katika kituo cha Afya Dongobesh, na hata mara nyingine kulazimika kupata matibabu katika hospitali ya rufaa Haydom na kushindwa kwenda huko kufuatia umbali uliopo na hivyo hali hiyo imekuwa ikiwaathiri na wakati mwingine kupelekea Vifo.
moja ya mashine zitakazotumika kufyatua matofali zikiwa eneo la ujenzi
Wakiongea kwa nyakati tofauti Mkuu wa Wilaya ya Mbulu ndugu Christino Mufoga,Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ndugu Joseph G. Mandoo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ndugu Hudson Kamoga,wamewashukuru Wananchi kwa kuhamasika na Kujitokeza kwa wingi katika hatua ya Awali ya Ujenzi huo, na huku wakiwaomba Wananchi kuendelea kujitolea kwa jinsi watakavyoweza na kuwa na dhamira ya dhati ya kusimamia mradi huo ili ujengwe kwa ubora kulingana na fedha zilizotolewa na Serikali na kukamilika kwa wakati ambapo unatekelezwa kwa nguvu za Wananchi yaani “Force Account”
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.