Aliyesimama ni Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndugu Hudson Kamoga Akiwa Katika Mkutano wa
Kusikiliza na Kutatua Kero za Wananchi Katika Mamlaka ya Upangaji ya Hydom tarehe 03.03.2021
Aliyesimama na Kushika "Mic" ni Mh. Mbunge Flatei wa Jimbo la Mbulu, Akisalimia Wananchi na Kutoa Ufafanuzi Juu ya Mustakabali wa Maendeleo ya Jamii Katika Jimbo la Mbulu na Hydom Kwa Ujumla wake.
Mh.Diwani Nasali Sule wa Kata ya Hydom Akitoa Ufafanuzi wa Maswala Mbalimbali Yaliyoulizwa Katika Viwanja vya Ofisi ya Kata ya Hydom
Aliyeshika "Mic" ni Mh.Mwenyekiti Elihuruma Manase wa Kijiji cha Hydom Akitoa Ufafanuzi wa Maswala Mbalimbali Yaliyoulizwa
Katika Viwanja vya Ofisi ya Kata ya Hydom
Aliyeshika "Mic" ni Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala Ndugu Horace Kolimba Akiwatambulisha Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri
ya Wilaya ya Mbulu Katika Mkutano huo, Viwanja vya Ofisi ya Kata ya Hydom.
Aliyesimama Kushoto ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Ndugu Sule Akiwasalimia Wananchi Katika Mkutano Huo.
Aliyesimama Kushoto ni Mratibu wa Mfuko wa BIMA ya Afya ya Jamii Ndugu Mtweve Akiwasalimia Wananchi Katika Mkutano Huo.
Aliyesimama Kushoto ni Mwakilishi wa Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi Akiwasalimia Wananchi Katika Mkutano Huo.
Aliyesimama Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Uchaguzi Ndugu M. Faray Akiwasalimia Wananchi Katika Mkutano Huo.
Wakwanza Kushoto ni Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndugu Hudson Kamoga Akitoa Maagizo Katika Mkutano wa
Kusikiliza na Kutatua Kero za Wananchi Katika Mkutano Huo.
Aliyesimama Kushoto ni Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Chitopela Akitoa ufafanuzi Katika Mada ya Idara Yake.
Aliyesimama Kulia ni Mwanasheria wa Wilaya Ndugu Mwambage Akitoa ufafanuzi wa Sheria.
Aliyesimama Mbele ni Mratibu wa Mpango wa Kusimamia Kaya Maskini wa Wilaya "TASAF" Ndugu Nguvava Akitoa ufafanuzi Katika Mada Iliyohusu TASAF.
Aliyesimama Mbele ni Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili Ndugu F. Kagenda Akitoa ufafanuzi Katika Mada ya Idara Yake.
Aliyesimama Kushoto ni Mkuu wa Idara ya MIfugo Ndugu Nduligu Akitoa ufafanuzi Katika Mada ya Idara Yake.
Aliyeshika "Mic" ni Mkuu wa Idara ya Afya na Usafi wa Mazingira Ndugu Kilimba Akitoa ufafanuzi Katika Mada ya Idara Yake.
Aliyeshika "Mic" ni Afisa Elimu Kata wa Kata ya Hydom Mkuu Ndugu Helen Massay Akitoa ufafanuzi Katika Mada ya Sekta ya Elimu Hydom.
Aliyeshika "Mic" ni Afisa Tarafa wa Tarafa ya Hydom Ndugu Benny Mwandelele Akitoa ufafanuzi wa Suala la Tozo za Mazingira.
Hizo Hapo Chini ni Baadhi ya Picha za Wananchi wa Hydom Waliotoa Kero Mbalimbali Zilizosikilizwa na Kujibiwa Hapo Hapo.
~~~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~~~
Hayo yamejiri leo katika mkutano mkuu wa wananchi ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji (W) wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndugu Hudson Kamoga, ambao uliofanyika katika viwanja vya ofisi ya Kata ya Hydom kuanzia saa tano asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni.
Kimsingi Mkurungezi huyu aliambatana na wataalamu wake wakuu wa Idara na vitengo vyote ili kutatua kero za wananchi wa Hydom pamoja na kutoa miongozo mbalimbali ya kiserikali ikiwemo sheria, afya, ardhi, mifugo, maendeleo ya jamii na kilimo.
Hata hivyo kikao hiki kimekuwa cha manufaa sana baada ya kila mwanachi aliyetaka kuuliza maswali aliuliza kisha ofisi ya mkurugenzi mtendaji ilitoa ufafanuzi wa kitaalamu hapo hapo wakati mengine yalipokelewa na kuendelea kuyafanyia kazi kwani yalihitaji ngazi zingine za maamuzi kama vile RUWASA, TARURA; muda na nyaraka zaidi.
Mkurugenzi Mtendaji, Ndugu Hudson Kamoga alitamka kwamba ni jukumu la kila mwananchi kila mwisho wa mwezi kufanya usafi katika eneo lake la biashara na nyumbani katika makazi yake, kila ofisi ya biashara kuhakikisha inakuwa na chombo cha kuwekea taka (dust bin) ili kurahisisha uzoaji wa taka hizo katika maeneo yote ya biashara na makazi. Serikali ya Kijiji cha Hydom iorodheshe majina ya wananchi wote waliohudumiwa na shirika la "FOCCP" lililokuwa linapima viwanja hapa kisha yaletwe ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ili taratibu za ufuatiliaji ufanyike baada ya wao hadi sasa kutojibu barua aliyowaandikia Shirika hili mwaka jana 2020.
Katika kujali wananchi na kukuza biashara Mkurugenzi Kamoga amesema, atahitaji kuwa na kikao na wafanya biashara wa Hydom kwani ni kitovu cha biashara katika Wilaya ya Mbulu kwa kuanzia na wamiliki wanaohusika na biashara za gesti ili kujua changamoto zao na kuweza kuzitatua kwani huu ndiyo utekelezaji wa Ilani ya Chama na Mapinduzi inayosimamiwa na kiongozi anayewajali wananchi na maendeleo yao Mh. Rais wa awamu ya tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. J. P. Magufuli.
Mgeni rasmi huyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Ndugu Hudson Kamoga aliongeza kwa kutamka kuwa mwananchi hana mipaka katika kutoa taarifa zake ili aweze kutatuliwa kero, hivyo akipiga simu ngazi ya kitongoji hajaridhika au kutopata majibu afuatilie ngazi ya Kijiji kisha kata hadi Tarafani akishindwa maeneo yote hayo basi apige simu ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
Katika kuhakikisha watumishi wa umma wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria; watumishi wote ni muhimu kuwa na lugha nzuri kwa wananchi lakini panapotokea lolote Afisa Mtendaji wa kata awawajibishe watumishi walio chini yake kwa mujibu wa sheria, tuwahudumie wananchi kwani sisi tuko kwa ajili yao na tunalipwa kwa kodi zinazotokana na kodi zao.
Ili kuwa na uwezo wa kufanya maendeleo mbalimbali ya kata na vijiji ni muhimu kuwa na takwimu sahihi ambapo imefahamika kwamba tayari Mamlaka ya upangaji ya Hydom wamejipanga kimkakati kupata idadi ya kaya sahihi na zoezi linaendelea ili isaidie katika kupanga na kufanya maamuzi mbalimbali ya maendeleo.
.
Kwa hali hii ili kudumisha utawala bora ni vizuri kila fedha zinapopatikana ni muhimu kuwapa taarifa wadau wakuu wa fedha hizi ambao ni wananchi wa kijiji au kata husika kupitia mbao za matangazo na mikutano mikuu ya vijiji kwa kusoma taarifa ya mapato na matumizi kila baada ya miezi mitatu ili kuwapa mrejesho wananchi na kujua fedha zimetumikaje, hii itaongeza imani ya wananchi katika serikali yao kuhusiana na uchangiaji chanya na endelevu wa miradi inayofuata.
Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu iko karibu sana na makundi maalumu ya Wanawake, Vijana na walemavu kwa kuwapa mikopo; aidha, kupitia fedha za marejesho tumetoa kiasi cha shilingi 121,277,893/= kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ikiwa ni vyanzo vya mapato ya ndani kwa 100% kwa lengo lililopangwa kwa vikundi 46, na mwaka huu wa fedha 2020/2021 unaoendelea hadi sasa tumetoa fedha kiasi cha shilingi 59,316,927/= kwa vingundi 15, na zoezi hili ni endelevu tunaendelea kutoa mikopo hiyo chamsingi ni kuandaa mihutasari ya vikundi na maandiko ya miradi husika kwa kupitia ngazi zote zinazohusika za mitaa kisha kufika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu pale Dongobesh ili kuweza kukamilisha zoezi la kupatiwa mikopo hiyo. Kuhusiana na michango mbalimbali Mgeni rasmi huo Ndugu Kamoga alimwagiza Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kukagua taarifa za michango ya wananchi na matumizi yake kuanzia wiki ijayokatika kijiji cha Hydom .
Katika kuupandisha hadhi Mamlaka ya Upangaji ya Mji wa Hydom na kuwa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Hydom bado vigezo havijafikiwa hivyo wananchi waendelee kuongeza juhudi za kimaendeleo kwa kuongeza kituo cha afya cha serikali hivyo muone mkakati wa kuleta mihtasari ya kituo cha afya cha serikali kwa kuainisha wapi eneo limepatikana lisilo na mgogoro na la ukubwa kiasi gani kisha tutashirikiana kwa pamoja kuona namna ya kupata fedha ili kituo kianze kujengwa mwaka huu 2021. Katika kufikia vigezo hivi ni pamoja na wananchi kupima na kulipia hati za viwanja vyenu ambapo ofisi mbalimbali na matumizi bora ya ardhi hupangwa, hadi sasa ujenzi wa Ofisi ya Mahakama ya Mwanzo unaanza ni mojawapo ya kushajiisha maandalizi ya mji huu.
Uongozi wa kata ya Hydom kupitia Mh. Diwani Nasaeli Safari Sule na viongozi wengine wa ngazi zote simamieni hili ili tuimarishe afya zetu kwa fedha kidogo kwa kituo cha afya cha serikali ukilinganisha na Hospitali ya sasa ya Hydom inayotoa huduma nzuri lakini gharama ni kubwa na pia ni hospitali ya rufaa hivyo inatakiwa kupunguziwa mzigo wa wagonjwa.Wananchi wote wa Hydom walimshukuru na kufurahi sana kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndugu Hudson Kamoga kwa Kuwa na Moyo wa Huruma kwa kuwajali, kuwafuata na Kuwasikiliza kero zao na kuzitatatua. Wananchi hao wamekiri kuyapokea maagizo yote na kuyafanyia kazi ipasavyo ikiwemo suala la ujenzi wa kituo cha afya cha Hydom. Mh. Mbunge naye alishukuru sana kwa Mkurugenzi Kamoga na menejimenti yake kusikiliza kero hizi kwani kwa hali hii maendeleo yatawezekana.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.