YAEDA CHINI-MBULU ��� 10 JUNI, 2023
Wito huo umetolewa mapema leo na Mkuu wa wilaya ya Mbulu Komred Kheri James,wakati akifunga mafunzo ya wiki mbili kwa viongozi na askari wa vijiji yenye lengo la kuwajengea uwezo na kuwapa ujuzi na mbinu za ziada katika jukumu lao la kulinda mazingira,na Kutunza hifadhi na wanyamapori.
Komred Kheri James amewasihi viongozi na wananchi wa vijiji vyote kuwapa ushirikiano wahitimu wa mafunzo hayo wanao tokea katika vijiji vyao ili tija ya mafunzo walio yapata iweze kuonekana.
Aidha Komred Kheri James amewaeleza viongozi na wananchi kuwa, utunzaji wa mazingira na uzingatiaji wa matumizi bora ya aridhi ni nyenzo muhimu ya maendeleo yao kiuchumi na kijamii, na hivyo amewataka kuzingatia utaribu waliojiwekea ili mazingira na maisha yao yaendelee kustawi.
Komred Kheri James amewapongeza sana uongozi wa Carbon Tanzania kwa kuamua kufadhili mafunzo hayo muhimu, ambayo yatachochea ufanisi wa uhifadhi.
Mafunzo hayo maalumu yamehusisha washiriki 139 kutoka Katika wilaya ya Mbulu na Karatu, ambao pia ni wanufaika wa biashara ya hewa ya ukaa inayo simamiwa na Taasisi ya Carbon Tanzania katika vijiji vyao.
Wilaya ya Mbulu inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika harakati za kutunza mazingira ili kupambana na mabadiliko ya Tabia ya nchi, na kuokoa uchumi na ustawi wa wananchi wanao ishi kwa kutegemea mazingira katika kilimo, mifugo na uwindaji.
#Kwapamoja,Tunaijenga Mbulu yetu.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.