Mwenyekiti wa Kijiji Cha Haydarer wilayani Mbulu mkoa wa Manyara Zebedayo Tambo akizungumza na wanakijiji wakati wa mkutano na wawezeshaji toka TASAF June 06,2023.
Mwezeshaji wa TASAF Christina Mgana, ametoa wito kwa wanufaika wa mradi wa TASAF Kijiji Cha Haydarer wajitahidi kufanya kazi na fedha wanazozipata wafanyie vitu vya msingi.
Bi. Christina alisema hayo wakiwa kwenye kikao na wanufaika wa mradi katika Kijiji Cha Haydarer wilayani Mbulu mkoa wa Manyara mnamo June 06,2023, wakikagua mradi uliopita wa upandaji miti na kujadili mradi Mpya wa Barabara.
Wanakijiji wa Haydarer Wilayani Mbulu wakiwa sikiliza wawezeshaji toka TASAF June 06,2023.
"Mradi huu wa Ajira za muda kwa walengwa ulianza kutekelezwa mwaka 2022 December,na tulianza na Mradi wa upandaji miti na sasa tumeanza mradi wa barabara ambao ni mradi wa pili." Alisema Bi. Christina.
Aidha Christina alisema kuwa kwa sasa wanapitia changamoto kubwa ya wanufaika hawalipwi kulingana na kazi wanazozifanya ambapo imepelekea wanufaika kulalamika kuhusu jambo hilo.
Hii ni barabara ambayo mradi wa pili unatarajia kuanza, Serikali ya Kijiji na wawezeshaji wa TASAF walipata wasaa wa kwenda kuikagua, June 06, 2023.
Kwa upande wa Mnufaika Bi. Bertha Sirili alisema kuwa mradi umemsaidia kwani tangu amejiunga na Mpango ameweza kumudu mahitaji muhimu kwa kusomesha watoto wake ambao bado wanaendelea na masomo.
Bi. Bertha alisema mbali na hayo Kuna changamoto wanayopitia ya kucheleweshewa malipo ama fedha zao kutokulipwa kwa wakati, hivyo ameiomba TASAF wajitahidi kuwalipa wanufaika kwa wakati.
Naye Mwenyekiti wa Kijiji Cha Haydarer bwana Zebedayo Tambo amewaomba wanakijiji anaowaongoza wajitahidi kufanya kazi kwa bidii ili wajikwamue kimaisha.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.