“Ufugaji wa nguruwe ni mojawapo ya mradi inayoinua pato la mtu binafsi, kaya,vikundina taifa kwa ujumla, hata hivyo mradi huu unakuwa unakwamishwa na mambo mbalilimbali yakiwemo magonjwa kwa wanyama”amesema hayo hii leo Dr. Ernatus M. Mkupasi alipokuwa akieleza juu ya tafiti.
Mnyoo Tegu unaojulikana kisayansi kama Taenia Soliumn ni moja ya matatizo makubwa yanayoathiri uzalishaji wa nguruwe nchini Tanzania kama ilivyo katika nchi zinazoendelea.
Binadamu na Nguruwe huambukizwa na huu mnyoo na kusababisha maradhi yanayopelekea kupungua kwa nguvu kazi na kushuka kiuchumi.
Ili kuepuka hayo yote Watafiti toka Chuo Kikuu cha Sokoine wamekuja na matokeo ya utafiti kwa kushirikiana na Mradi wa Cysticercosis Network of Sub - Saharan Africa (CYSTINET- Africa) uliolenga kuelimsha jamii jinsi ya kuzuia na kudhibiti Mnyoo Tegu kwa kutumia mbinu iitwayo Afya Shirikishi na hatimaye kuboresha afya za binadamu kwa ujumla,kulinda mazingira na kuinua uchumi wa wafugaji pamoja na wadau wote wa sekta ya mifugo
Utafiti huu umefanyika hapa nchi kwa maeneo mbalimbali, miongoni mwa Mikoa iliyofanyiwa tafiti ni Manyara, Dodoma, Mbeya ,Singwe , Iringa,Njombe na Ruvuma na maeneo hayo yote yalibainiki kuwa na maambukizi.\
Aidha kwa Mkoa wa Mnayara uatfiti huu ulifanyika kwa Wilaya ya Mbulu na Babati, katika Wilaya ya Mbulu utafiti ulifanyika kwa maeneo ya Masieda na Maghang.
Ili kuendelea kudhibiti kuendelea kwa maambukizi ya minyoo tegu kwa binadamu na nguruwe tunashauriwa kuzingatia mambo yafuatayo:
Kuzingatia matumizi sahihi ya Choo.
Kuimarisha usafi wa mtu binafsi na Mazingira
Kuzingatia usalama wa vyakula, ikiwa ni pamoja na kunywa maji safi na salama
Kukagua Nyama ya Nguruwe kabla ya matumizi
Kuzuia ufugaji huria wa Nguruwe
Kuendelea kutoa elimu enedelevu ya maambukizi ya Minyoo ya Tegu
Pia kuendelea kutumia mbinu ya Afya shirikishi katika mapambano ya minyoo.
Tukiungana na kuzingatia elimu mbalimbali inayotolewa na wataalamu hakika tutatokomeza minyoo hao.
KWA PAMOJA TUNAIJENGA MBULU YETU.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.