Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu akisisitiza jambo ndani ya kikao kazi cha Watendaji wa Kata na Vijiji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Mbulu, ndugu Hudson Kamoga amewataka Watendaji wa kata na Vijjji kusimamia Ukusanyaji wa Mapato yatokanayo na vyanzo vya ndani kwa Ufasaha na kwa kasi zaidi ili kufikia lengo lilokusudiwa na halmshauri kwa mwaka fedha 2108/2019,ameyasema hayo hii leo katika kikao kazi kilichojumuisha Wataalam wa halmashauri na Watendaji wa Vijiji 76,Kata 18 ndani ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri.
Ndugu Kamoga amewataka Watendaji wote kuwa chachu ya kusimamia Mapato na Matumizi kwa kila Mtendaji wa Kata na Kijiji uku akisisitiza uwazi na ukweli wa fedha zote zinazokusanywa ndani kata au kijiji husika kwa kuepuka kesi zisizokuwa na sababu.
Mkurugenzi akiwa meza kuu pamoja na maafisa utumishi, toka kulia ni Eliah Samata(afisa utumishi), Horace Kolimba( Afisa Utumishi Mkuu), Magreth Masawe(Afisa Utumishi) na Chamba Kajeri.
“Kikao hiki mmeitwa hapa kwa lengo la kukumbusha majukumu yenu ya kila siku na ndio maana hii leo Wataalam toka kila Idara na Vitengo wataongelea kila mmoja sehemu ya majukumu yake”.alisema Kamoga.
Aidha Mkurugenzi amesisitiza kufuatilia kwa karibu zaidi Mapato yanayokusanywa ndani ya kata/ kijiji husika na kuhaidi kuwanunulia vifaa vya kukusanyia mapato (POS) ili kila chanzo kinachokusanywa kiwe kimepitia mfumo sahihi wa ukusanyaji.
Baadhi ya Watendaji wa Vijiji wakiwa katika kikao, kutoka kushoto ni Bi.Sentala L. Katule Mtendaji wa Kijiji cha Basoderer,Mariam A. Songoro Mtendaji wa Kijiji cha Qatabela, na Bi. Rachel C. Patrick Mtendaji wa Kijiji cha Garbabi
Ndugu kamoga ametoa pongezi wa Watendaji wale wote wanaokuwa wepesi kutoa taarifa ya kimandishi ofisini kwake pale wanaposhindwa kusoma taarifa ya Mapato na matumizi kwa wakati, na kutoa wiki mbili kuhakikisha kila kijiji kiwe kimekamilsha taratibu zote za ufunguaji wa akaunti kwa ajili yakuingiziwa fedha za mfuko wa jimbo kwa maendeleo ya kijiji.
Mtendaji wa kijiji cha Harsha ndugu Isaya M.Kazi wa kwanza kulia na ndugu Malkiadi J. Haqwet Mtendaji wa kijiji cha Gidhim wakiwa katika kikao kazi hii leo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Mhe Joseph Mandoo amewataka kila Mtendaji wa kata na kijiji kuhakikisha wanakuwa na Sheria ndogo zilizopitishwa na vikao halali vya halmashauri zitakazowalinda pindi wanapoenda kukusanya mapato na hata kutoza faini ziwe za halali. Pia mwenyekiti amewataka watendaji kuwa wasimamizi wa karibu kwa miradi inayoendelea ndani ya eneo husika uku akiwataka wasisite kutoa taarifa pale wanapoona mradi unaondelea hawajaridhishwa na mwenendo wake.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.