Akiongea katika kikao cha tathimini ya hali ya lishe ya chakula cha halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kilichofanyika hii leo tarehe 23/06/2023, Komredi Kheri James Mkuu wa Wilaya ya Mbulu ameipongeza halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kwa kutoa fedha kwa asilimia mia(100) ili kuweza kusaidia maswala ya lishe kwa watoto walio chini ya miaka mitano(5).
Kikao hicho kimehudhuriwa na Wajumbe mbalimbali toka halmashauri, kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya,pamoja na Watendaji wote wa kata 18 za halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
Pamoja na tathimini iliyotelawa na Mganga Mkuu wa Wilaya ikionesha hali ya lishe na utoaji wa Elimu ya lishe kwa kata tisa za halmashauri ya Wilaya ya mbulu tumefikia kiwango cha asilimia 50 na mikakati mbalimbali ikiendelea kuwekwa kufikia malengo, Mkuu wa Wilaya ya Mbulu awaagiza Watendaji kuhakikisha wanasimamia na kutekeleza mambo mbalimbali ili kuweza kufikia malengo.
Komredi James awataka Watendaji Kuendelea kusimamia mpango wa lishe bora mashuleni, ikiwa ni pamoja na kuhimiza shule zote katika halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kuanzisha bustani za mboga mboga aina mbalimbali pamoja na upandaji wa miti ya matunda.
Kusimamia unywaji wa maji safi na salama mashuleni baada ya mlo, ili kupunguza magonjwa ya mlipuko katika Wilaya yetu na Kuendelea kuielemisha jamii ngazi ya vijiji na vitongoji hasa kaya zenye watoto chini ya miaka mitano juu ya umuhimu wa lishe bora.
Aidha, amesisitiza maafisa kilimo watoe elimu kwa wakulima juu ya upandaji wa mazao ya lishe, ikiwa ni mahindi na maharage lishe pamoja na uoandaji wa bustani za mboga mboga na matunda kwa wingi,pia itolewe kwa wenyeviti wa vitongoji, wahudumu wa afya ngazi yajamii, kanisani na misikitini, ili waendelee kuhimiza na kutoa elimu ya lishe bora hata katika nyumba za ibada.
Hakihitimisha kikao hicho cha tathimini Komredi Kheri James amewataka watendaji wa kata wawe na utamaduni wa kutembelea mashuleni ili kuangalia aina ya vyakula ambavyo wanafunzi wanandaliwa pamoja na mazingira ambayo chakula kinaandaliwa kama ni safi na salama
#KWA PAMOJA TUNAIJENGA MBULU YETU.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.