Ndugu Wazazi,Walezi na Watoto
Nimefurahi kupata nafasi hii ya kuwa Mgeni Rasmi katika maadhimisho haya ya siku ya Mtoto wa Afrika yanayoadhimishwa kwa halmashauri yetu hapa Hyadom. Lakini pia nimefurahi kuona maandamano,maonyesho, vipaji mbali mbali vya watoto zikiwemo nyimbo, maigizo,sarakasi na Mashairi. Nawapongeza sana kwa wale watoto walioonesha vipaji vyao na natoa wito kwa Idara ya maendeleo ya jamii kuendelea kuvilea, kuviendeleza na kuvikuza vipaji hivi ili baadae watoto pamoja na Taifa letu liweze kunufaika na vipaji hivi. Aidha, nimesikia Risala ya watoto ambayo imejumuisha haki za kimsingi za watoto ambayo imebainisha wazi changamoto wanazopitia watoto wetu, Alisema hayo ndugu Abubakar Kuuli Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu. Nipende kuchukua fursa hii kuwakumbusha chimbuko la maadhimisho haya,
“Kila mwaka tarehe 16 Juni Tanzania inaungana na Nchi zingine za Afrika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika.Chimbuko la Maadhimisho haya ni Azimio lililopitishwa na uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) mwaka 1990 kwa lengo la kuwakumbuka watoto wa kitongoji cha Soweto nchini Afrika ya Kusini waliouawa tarehe 16 Juni, 1976 kutokana na ubaguzi wa rangi”.
Watoto hao walikuwa wakidai haki zao za kutobaguliwa pamoja na haki nyingine za kibinadamu ikiwemo haki ya kupata elimu bora na hivyo kupinga mifumo ya elimu ya kibaguzi. Kufuatia tukio hili, OAU iliazimia kuwa tarehe 16 Juni ya kila mwaka iwe Siku ya Mtoto wa Afrika.
Kupitia Maadhimisho haya nipende kuwakumbusha kuandaa mipango thabiti ya kuwaendeleza watoto na kukuza ufahamu wa wazazi, walezi na jamii kuhusu kuzingatia usalama wa Mtoto katika Ulimwengu wa Kidigitali
Aidha, maadhimisho haya ni fursa ya kutathmini utekelezaji wa Sera za Taifa zinazohusu maendeleo ya watoto kwa kuwapatia huduma stahiki ikiwa ni pamoja na afya, elimu, ulinzi na malezi bora ili kuwarithisha stadi mbalimbali na tunu za kitaifa kwa manufaa yao, familia na taifa kwa ujumla.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni “kuzingatia usalama wa Mtoto katika Ulimwengu wa Kidigital” Kauli mbiu hii inawataka wazazi, walezi, Serikali na wadau wengine kuzingatia wajibu wetu katika kuimarisha mifumo ya ulinzi na maendeleo ya Mtoto ili aweze kudhibiti changamoto ya ongezeko la vitendo hatarishi katika ulimwengu huu wa kidigitali pamoja na kutoa haki sawa kwa watoto wote bila ubaguzi wa aina yoyote.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.