Aliyeshika Mwenge Kushoto ni Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt, C. Mofuga Akipokea Mwenge wa Uhuru Kutoka Kwa (kulia) Mh. Mkuu wa Wilaya ya Hanang katika Kijiji cha Endegew
Katikati Aliyeshika Kipaza Sauti (mic) Kiongoziwa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2021 Luteni, Josephine Paul Mwambashi Akizungumza na Wananchi Katika Mradi wa Maji Dongobesh Kata ya Dongobesh, Kushoto ni Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt, C. Mofuga na Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Hudson Kamoga.
Uzinduzi wa Daraja la Masigeta Kijiji cha Geterer
Kuona Shuguli za Klabu ya Wapinga Rushwa na Klabu ya Ukimwi Shule ya Sekondari Dr.Olsen
Kutembelea na Kuona Shuguli za Uchakataji wa Mradi wa Lishe na Maziwa Chuo cha Tango
Picha za Hapo Chini ni Mabanda Mbalimbali Uwanja wa Daudi Kata ya Daudi
Bw. Silvanus Rweymamu Akitoa Ufafanuzi Katika Banda la Falsafa
Aliyeshika Kipaza Sauti (mic) ni Bw. Michael Mwalyambi Afisa Tehama Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Akitoa Ufafanuzi Katika Banda la Falsafa Upande wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
Banda la Benki - Benki Mtandao
Aliyevaa Fulana Nyeupe Kushoto ni Bw. Tembe, Afisa Tehama Mbulu Mjini Akiweka Vitu Sawa Katika Banda la Falsafa Upande wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
Banda la Falsafa ya Mwenge na TEHAMA - PESA Mtandao na Matumizi ya Mashine za Kukusanyia Mapato "POS" Serikalini
Banda la KILIMO Kampuni ya Seed-CO
Banda la Uelimishaji na Ufuatiliaji wa Madawa ya Kulevya
Banda la Damu Salama na Kupambana Zidi ya Malaria
Banda la TAKUKURU
Burudani ni Nyumbani
Katibu Tawala Wilaya ya Mbulu. Ndugu Sara Sanga Akisoma Salamu ya Utii kwa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia S. Hassan
Makabidhiano ya Mwnge wa Uhuru Leo Tarehe 16.06.2021 Uwanja wa Kansai Kijiji cha Barakta Wilayani Karatu, Mkoani Arusha na
(kulia) Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara M.Nyerere kwa Kumkabidhi (kushoto) Mh. Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mongera
~~~~~~~~~~~~~~~~~ HABARI KAMILI ~~~~~~~~~~~~~~~~~
Haya yamejiri jana tarehe 15.06.2021 baada ya Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Mh. Luteni J.P.Mwambashi kuridhika na kuridhia kuzindua, kuona, kufungua, kutembelea na kukagua shuguli mbalimbali mtambuka na miradi ya sekta kadhaa ikijumuisha elimu, afya, maji, barabara, mifugo, ardhi na TEHAMA yenye thamani ya Tsh. bilioni 1,274,57,646.00 kwa mchanganuo wa Tsh. milioni 61,881,500.00 ikiwa ni nguvu za wananchi, Tsh. bilioni 1,155,481,946.00 serikali kuu, Tsh. milioni 2,070,000.00 Halmashauri na wahisani Tsh. 54,624,500.00.
Mwenge wa uhuru wa mwaka 2021 umepokelewa jana tarehe 15.06.2021 katika eneo la mapokezi na makabidhiano ya mwenge wa uhuru kijiji cha Endegew uwanja wa shule ya Sekondari Geterer, kisha shuguli mbalimbali za mwenge huo zilifuata ; Uzinduzi wa daraja la Masigeta kijiji cha Geterer, kuona shuguli za klabu ya wapinga rushwa na klabu ya ukimwi shule ya sekondari Dr.Olsen, Ufunguzi wa mradi wa maji Dongobesh kata ya Dongobesh, kutembelea na kuona shuguli za uchakataji wa mradi wa lishe na maziwa chuo cha Tango, uwanja wa mbulu mjini kutoa hati za urasimishaji za viwanja vya kata ya Ayomohe na Sanu kwa wananchi, uwekaji wa jiwe la msingi zahanati yaBarigish Uwa katika kijiji cha Bargish uwa, kukagua na kuona uendelevu wa mradi wa maji wa 2019 kijiji cha Bargish Antsi na ukaguzi wa matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa serikali wa kukusanya mapato ya hospitali (GOTHOMIS) katika Kituo cha Afya cha Daudi kijiji cha Moringa.
Baada ya zoezi hilo kuisha mwenge wa uhuru uliingia katika uwanja wa kata ya Daudi kwa lengo la kukagua mabanda ya TEHAMA, Malaria, Madawa ya kulevya, falsafa ya mwenge, banda la shuguli za ukimwi na lishe mambo ambayo kiongozi wa mbio za mwenge na wakimbiza mwenge alilokuwa na walifurahishwa sana kwa maandalizi ya kutosha kwa kuwepo vifaa husika, watumishi waoajitambua katika kujieleza na muoundo wa kila kitu kilichokuwepo kwa kila banda na katika hili alishukuru sana kwa Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu. Dkt. C.Mofuga.
Pamoja na kupitia miradi ya maendeleo, mwenge wa uhuru umekimbizwa ukiwa unaeneza ujumbe wa matumizi ya TEHAMA ni msingi wa taifa endelevu itumie kwa usahihi na uwajibikaji
Baada ya hapo hoihoi, nderemo na vifijo viliendelea kwa burudani kali ya aina yake ambapo wananchi wa wilaya ya mbulu walijaa pomoni kwa ushajiishaji wa miziki ya kizazi kipya maarufu "bongo flavour", milindimo ya kikongo, ngoma za asili vichekesho na mazoezi mbalimbali ya vijana kama vile sarakasi na vingine vingi vilivyotoa shangwe katika mkesha wa mwenge wa uhuru wa mwaka 2021 uwanja wa kata ya Daudi.
Mwisho Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Dkt C. Mofuga kwa niaba ya wananchi wa Wilaya ya Mbulu amesema "tunaishukuru serikali na wadau wengine kwa kutoa fedha mbalimbali za miradi hii ambayo ni chachu ya maendeleo kwa wananchi na Taifa letu kwa ujumla wake".
Mwenge huo umekabidhiwa leo tarehe 16.06.2021 uwanja wa Kansai Kijiji cha Barakta Mkoani Arusha na Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara M.Nyerere kwa Kumkabidhi Mh. Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.