Mkuu wa wilaya ya Mbulu Komred Kheri James, ametoa maelekezo kwa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu, kuhakikisha kuwa Zahanati zote zilizo Jengwa na kukamilika zianze kutoa huduma ili kutimiza lengo la kujengwa kwake na kuwarahisishia huduma Wananchi.
Akizungumza na Wananchi katika ziara yake katika Kata ya Masqaroda na Bashay, Komred Kheri James ameeleza kuwa lengo la Serikali la kujenga Vituo vya Afya na Zahanati ni kusogeza na kurahisisha huduma za Afya kwa Wananchi, ambao wanafata huduma maeneo ya mbali na kwa gharama kubwa. Hivyo amesisitiza kuwa ni muhimu kila ujenzi wa mradi wa afya unapo kamilika,Vifaa na Watumishi Wapelekwe ili huduma zianze kutolewa kwa Wananchi.
Katika ziara hiyo Komred Kheri James ametembelea miradi ya Elimu, Afya na Maji yenye thamani ya shilingi Milioni mia Saba Thelathini.
Pamoja na mambo mengine ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kwa kukamilisha miradi hiyo na amewashukuru Wananchi na Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Ndugu Flatei Massay kwa Juhudi zao katika kuchangia miradi ya Maendeleo.
Mkuu wa wilaya ya Mbulu Komred Kheri James anaendelea na ziara ya kukagua miradi ya maendeleo, kuhamasisha Shughuli za maendeleo na kusikiliza kero za Wananchi katika Kata zote za wilaya ya Mbulu, na kwasasa yupo katika Kata za Halimashauri ya wilaya ya Mbulu.
#Kwapamoja,Tunaijenga Mbulu yetu.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.