Picha Inayoonekana ni Wazazi Wakiwa na Watoto Wao Katika Ofisi ya Kata ya Haydom Wakiwa Katika Hatua za Usajiri Ili Waweze Kupata Cheti Kwa Watoto Wao Mbele ya Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Waliopewa Mafunzo Elekezi ya Namna ya Usajili na Kutoa Cheti Kupitia Ujazaji wa Fomu Maalumu na Kisha Kuzipakia Kwene Mfumo wa Kielektroniki wa Usajili.
Kikosi Kazi cha Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Kinachosimamia Zoezi Zima la Usajili na Utoaji Vyeti Ambapo Hapo Kuna Makundi Matatu Kundi la Kwanza ni la Wasimamizi wa Taasisi ya "RITA" Ngazi ya Kitaifa, la Pili ni Maafisa Kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbulu na Tatu ni Wataalamu Kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
Picha ya Hapo Juu ni Watumishi Mbalimbali Wakiwa Katika Zoezi la Kupakia Taarifa za Usajili Kwa Kutumia Mfumo wa Kielektroniki Uliopo Kwenye Simu.
Katika Kila Kazi Kuna Changamoto Mbalimbali Ambazo Kikosi Kazi Hiki Kinakumbana Nazo Mojawapo ni Kuharibika kwa Usafiri Unaotumika Katika Kazi Hii AMbapo Imebidi Wao Wenyewe Kurekebisha Athali Hizo Ili Waweze Kuendelea na Zoezi Bila Kuathili Kazi ni Uzalendo wa Kutosha Katika Hili.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~` TAARIFA KAMILI ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Ili kuhakikisha haki ya mtoto inatunzwa na kumuandaa mtoto katika baisha bora na ya mafanikio katika elimu na biashara na mengineyo ya kijamii kwa ujumla wake serikali imetekeleza kwa vitendo na sasa ndicho halisia katika zoezi la uandikishaji.
vituo vinavoendelea na zoezi hili ni 44 kwa wilaya nzima ambapo kwa ngazi ya Kata ni 18 kwa majina ni kama ifuatavyo:-
Bashai, Endamilay, Dongobesh, Dinamu, Endahagchan, Tumati, Yaedachini, Masqaroda, Maghan, Maretadu, Haydarel, Geterer, Haydom, Eshkesh, Masieda, Gidhim na Labay.
Katika sehemu za kutolea huduma za afya Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati ni kama ifuatavyo:-
Yaedaampa, Maghan, Masqaroda, Arri, Muslur, Yaeda chini, Tumati, Masieda, Endamilay, Bashai, Diyomati, Dirim, Dongobeshi kituo cha Afya, Endahalghadat, Ngorot, Gidmadoy, Labay, Harbangheti, St.Alois Hospitali, Hospitali ya Haydom, Huruma, Maretadu Juu, Haydarer, Endamasak, Maretadu Chini, Mewadani na Endoji.
Katika zoezi hili changamoto ni za kawaida ikiwemo kuisha kwa vitabu vya kuandikishia ambapo wahusika wa kituo husika wakitoa taarifa hufikishiwa mara moja ili kuokoa muda kutoka wasimamizi ngazi ya Taifa na Wilaya.
Hata hivyo changamoto ya barabara imekua kubwa kidogo kwa baadhi ya maeneo ambapo kinachofanyika wataalamu hufika kwa muda ambao sio mwafaka kutokana na miundombinu hafifu ya barabara hii imepelekea kufanya ufukuaji na matengenezo ya mara kwa maramara tuwapo kwenye mzunguko wa usimamiaji wa kazi hii.
Wataalamu wetu wamejitoa kwa weledi wote na nguvu zote kuhakikisha kila kitu kinakwenda vizuri na kufikia malengo yaliyopangwa.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.