Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan ameanza ziara ya kiakzi Mkoani Manyara leo tarehe 14/11/2018 akitokea Mkoani Kiliamnajaro na kupokelewa katika Mji mdogo wa Mirerani Mkoani Manyara.
Akimkaribisha Mkoani Manyara wakati wa kumpokea Makamu wa Rais katika Mji mdogo wa Mirerani Wilayni Simanjiro Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh.Alexender Mnyeti alisema kuwa Mkoa wa Manyara umepata maendeleo katia sekta mbalimbali mbalimbali ikiwemo Kilimo,Miundombinu,Elimu,Madini,Afya,Maji n.k
“Mh.Makamu wa Rais kwa sasa Mkoa wa Manyara unaendelea kuhakikisha dawa na vifaa tiba vinakuwa vya kutosha katika vituo vyote vya kutolea huduma kwani kwa sasa bajeti ya dawa imeongezeka hadi kufikia asilimia 93.9 yaani kwa kifupi Dawa zinasubiri wagonjwa” Alisema Mh.Mnyeti.
“Mkoa wa Manyara umejenga vituo vya Afya saba katika Wilaya zote zilizopo katika Mkoa huo na vituo hivyo vinatarajiwa kuanza kutoa huduma kwa wananchi kuanzia tarehe 30 Novemba 2018” Mheshimiwa Mnyeti alisisitiza.
Katika sekta ya Madini Mkuu wa Mkoa wa Manyara alisema kuwa Mkoa umebarikiwa iana mbalimbali ya madini kama Tanzanite,Tsavorite,Toummaline,Rhodolite,Grossulanite,Lolite,Limestone n.k.
Akizungumzia faida iliyopatikana baada ya kujengwa ukuta katika machimbo ya Mirerani Mkuu wa Mkoa wa Manyara alisema “Mhesimiwa Makamu wa Rais Miezzi kumi kabla ya kujengwa ukuta mapato yalikuwa milioni 400 lakini miazi kumi baada ya ukuta kujengwa mapato ni Bilioni 2.1 hii ina maana mapato yameongezeka kwa asilimi 425”
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ndugu Hudson Stanley Kamoga( Mwenye koti la Suti la kijivu) pamoja na Mkurugenzi wa Mji wa Mbulu, Bi Anna Mbogo (aliye karibu na afande Uhamiaji) wakisikiliza kwa makini hotuba ya Makamu wa Rais
Akiongea baada ya kupokea ripoti ya Mkoa Makamu wa Rais alisifu juhudi mbalimbali zinazofanywa na Mkoa katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Mkoa wa Manyara.
Pamoja na pongezi hizo lakini pia Makamu wa Rais aliwataka viongozi wa Mkoa wa Manyara kuongeza juhudi katika suala la lishe ili kuondokana na udumavu, vilevile alizitaka mamlaka za serikali za mitaa kufanya juhudi katika kupiga vita juu ya maambukizi ya UKIMWI “Japokuwa Mkoa wa Manyara ni Mkoa wa tatu kutoka mwisho bado juhudi zinahitaji ili kusiwe na maambukizi mapya” Alisistiza Makamu wa Rais.
Ziara ya Makamu wa Rais itaendelea kesho kwa kutembelea Ukuta wa Mirerani, Kufungua Kiwanda cha Graphite na kufanya Mkutano wa hadhara huko Orkesumet Wilaya ya Simanjiro.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.