Na Ruth Kyelula, Afisa Habari Mbulu DC,
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, ndugu Moses Nduligu, amezindua kampeni ya Kitaifa ya utoaji wa Chanjo ya Surua na Rubella kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano ambayo imeanza kutolewa tarehe 15 hadi 18, Februari, 2024.
Kaimu Mkurugenzi alizindua chanjo hiyo jana Februari 15,2024 katika kituo cha Afya Dongobesh, kilichopo katika Wilaya ya Mbulu.
“Tupo hapa kwa ajili ya zoezi la uzinduzi wa chanjo, maana yake zoezi hili linaendelea katika vijiji vyote vya Halmashauri yetu ya Wilaya ya Mbulu, Halmashauri yetu ina vijiji 76, lakini Mganga Mkuu ameamua tufanye uzinduzi katika kata yetu ya Dongobesh na kwenye kituo cha Afya Dongobesh.Kwahiyo sisi tumepata bahati ya kupata uzinduzi huu, na kwa maana hiyo sisi tunatakiwa tuoneshe lengo lililokusudiwa na Serikali kwenye eneo letu.” Alisema Nduligu.
Kaimu Mkurugenzi, Moses Nduligu akitoa salamu za Serikali kwenye uzinduzi wa chanjo ya Surua Rubella.
Aliendelea kusema kuwa chanjo hizi ni muhimu sana kama wataalamu walivyosema, na chanjo zote Duniani zinamalengo ya kuzuia magonjwa. Yani maana yake ukipata chanjo wewe hautaugua ugonjwa huo. Kwahiyo ukiona Serikali inatoa gharama hizi zote, maana yake inaona umuhimu wa zoezi hili kwa Wananchi wake.
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya Martin Mwandiki alisema kuwa, watashukuru wakina mama wakiwaleta watoto wapate chanjo kwa wakati, ili wawakinge na magonjwa. Kwahiyo tuhimizane huko majumbani watu walete watoto wapate chanjo.
Mganga Mkuu wa Wilaya, Dkt. Martin Mwandiki akizungumza na wakina mama wa kata ya Dongobesh waliojitokeza kwenye zoezi la chanjo
Kwa upande wake Afisa Afya na Mratibu wa huduma za chanjo Ali Suleiman, alisema kuwa kuna zoezi la kampeni ya kitaifa ya utoaji wa chanjo ya Surua Rubella pamoja na chanjo nyingine, vile vile utoaji wa matone ya vitamin A, kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano. Na zoezi hili linafanyika Nchi nzima, Tanzania bara.
Baadhi ya wakina mama wa kata ya Dongobesh, waliojitokeza kwenye chanjo
“Jamani hizi chanjo ni muhimu, zinaongeza kinga katika mwili na zinasaidia kukinga magonjwa mbalimbali kwa mujibu wa chanjo husika. Lakini chanjo ya Surua inawakinga walengwa ambao wamepatiwa chanjo na ugonjwa wa Surua. Surua ni hatari,Surua inaua.” Alisema Afisa Afya.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.