Kulia ni Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Sezaria V. Makota na Kushoto ni Katibu Tawala Wilaya ya Mbulu S.Sanga
Dereva Hanbeti Akiwa Katika Zoezi la Anwani za Makazi Katika Kusambaza Miti Kupeleka Sehemu Mbalimbali ya Kata Kwenye Upungufu wa Vifaa Hivyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Abubakar A. Kuuli Aonyesha Mfano kwa Vitendo Katika Zoezi la Anwani za Makazi Katika Halmashauri yake
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Dongobesh Akisimamia Kazi Yake Usiku Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Abubakar A. Kuuli Usiku Kucha Akiwa na Watendaji Katika Kuhakikisha Nguzo Zinapatikana kwa Wakati.
Haya yamejiri tarehe 28.05.2022 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ambapo Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji, Wenyeviti wa Vitongoji na Vijiji, Madiwani na Wakuu wa Idara/Vitengo kwa nguvu moja wanaendelea na zoezi hili kuhakikisha hakuna kulala hadi kazi ikamilike kama ilivyoagizwa na Mhe.Rais S.S.Hassan .
Kimsingi hadi leo mchana 70% ya kata zote zoezi lilikuwa ni jukumu moja tu japo kwa hatua mbalimbali za ukamilishaji ambapo ubebaji, kuchana mbao, kutengeneza nguzo, kuchimba na kusimika nguzo za barabara vinafanyika ili Jumapili asilimia ilobaki itimie.
Mhe. Mkuu wa Wilaya huyo aliongozana pia na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Abubakar A. Kuuli, Baadhi ya maeneo aliyotembelea ni pamoja na Dongobesh Chini, Dongobesh, Qaloda, Masqaroda, Bashay, Yamai na mengine mengi, ambapo katika Kijiji cha Dongobesh.
Hata hivyoMhe. Mkuu wa Wilaya huyo aliongozana pia na Mkurugenzi Mtendaji (W) ndugu A. A.Kuuli alishiriki katika zoezi la kuandika maandishi mbalimbali katika vibao vya nguzo za barabara za Dongobesh. Haikuishia hapo tu kwani ukaguzi uliendelea hadi usiku huu ambapo Maafisa wetu wa Kata na Vijiji wanapiga kazi nzuri usiku na mchana ili kuhakikisha kazi inakamilika kama ilivyopangwa na tutafanikiwa.
Akiwa katika zoezi la ukaguzi wa zoezi la anwani za makazi ambalo amekuta liko katika hatua mbalimbali kwa Kata tofauti, Mkurugenzi huyo ametoa magari kadhaa kwa ajili ya kurahisisha kubebea miti ambayo ilikuwa inapatikana katika jengo la Halmashauri na kupelekwa kwenye maeneo yote yaliyokuwa yamepelea miti kiasi kwamba hali imekuwa shwari na jumapili ya tarehe 29.05.2022 itakuwa ni kazi nyepesi ya kukamilisha maeneo machache yaliyosalia.
Wito wa Mhe. Mkuu wa Wilaya S.V.Makota amesema "Maafisa wote wanaohusika na kazi ya anwani kuanzia makao makuu ya Wilaya, Timu ya Napa ya Wilaya, Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji, Wenyeviti na wananchi kwa ujumla wao wajitume katika kazi hii kwa faida yao wenyewe.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.