Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu azindua mashindano ya KURUGENZI CUP'18 katika mji wa Haydom yanayokutanisha timu mbalimbali, uzinduzi huu umefanyika ikiwa ni wiki ya Ujasiliamali,Uwajibikaji na Uzalendo kuelekea Tanzania ya Viwanda.
akiongea na mamia na wananchi waliojitokeza amewataka kuwa wazalendo kwa kupigania nchi yao nakuonesha mshikamano katika kujiletea maendeleo yao.
aidha amewakumbusha kuitumia mbulu kwa fursa zake zilzipo ili kuisaidia mbulu kusonga mbele.
Mkurugenzi Mtendaji ametoa ushauri kwa watu wote kupunguza lawama kila unapofanya jambo/kazi na hata kudumaza uwezo wa kufikiri https://www.youtube.com/watch?v=7-LkFKuX9RA&feature=youtu.be
Aliyekuwa Diwani wa kata ya Hayderer Wilaya ya Mbulu,Mh. Justine S. Masuja kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ameamua kujivua Madaraka yake ya Udiwani na kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM) ili kuendana na Sera za awamu ya tano .
Ametoa maamuzi hayo mbele ya wananchi Wilayani Mbulu hivi karibuni , mara baada ya kukaa na kutathimini mustakabali wa kisiasa nchini akiongea dhumuni kubwa la kujiudhuru nikutokana na kufanya maamuzi yake kwa hiari pasipo kushirikishwa na mtu au kushawishiwa na mtu yoyote.
Akiongea zaidi ameahamua kuunga mkono harakati zinazofanywa na Mhe. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli za kupambana na mafisadi, rushwa na kuwaletea wananchi maendeleo Tanzania.
Aidha kuhamua kujiunga na chama cha Mapinduzi kutokana na kushindwa kutekeleza ilani ya chama cha Mapinduzi huku akiwa upinzani.
“Nimeamua kuwatumikia wananchi wangu wa Hayderer kwa dhati ili kuwaletea maendeleo nikiwa natekeleza Sera za Awamu ya Tano kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM). Alisema Masuja’.
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.