Na Ruth Kyelula, Mbulu DC
Kaimu Meneja wa Birth Hope Center, Mariam Fanuel amewataka wasichana wa shule ya msingi Dongobesh Viziwi kuwa wasikate tamaa na wajione kama wanawake wengine na wanathamani katika jamii lakini pia wafanye jitihada Zaidi katika masomo yao ili wafikie ndoto zao.
Hayo yalisemwa na Kaimu Meneja wa Birth Hope Center, Mariam Fanuel wakati walipoenda kutembelea shule ya Dongobesh viziwi na shule ya secondary Bashay, kugawa taulo za kike mia tatu (300), zilizopo Wilaya ya Mbulu, Mkoa wa Manyara, Novemba 4,2024.
Wanafunzi wa Dongobesh viziwi wakifuautilia maelekezo ya namna ya kutumia taulo walizopewa.
“matukio kama haya yatakuwa endelevu kwa jamii zote zenye uhitaji, na wote ambao wanawiwa kuungana nasi kwenye matukio kama haya tunawakaribisha tuungane kusaidia watu wenye uhitaji kwenye Wilaya yetu.” Alisema Mariam.
Kwa upande wa mwalimu mkuu wa shule ya msingi Dongobesh Viziwi, Veronica Joseph ameiomba serikali na wadau wengine wawe wanaitembelea shule hiyo mara kwa mara ili kuwasaidia watoto hao wenye nahitaji maalumu.
Pia amewaomba wanafunzi wasiache shule kwa ajili ya hedhi, bali wapatapo changamoto yoyote wasisite kuwashirikisha walimu ili wajue namna nzuri ya kuwasaidia.
Wanafunzi wa Dongobesh Viziwi wakielekezwa namna ya kutumia taulo walizopewa
Aidha wanafunzi wa Dongobesh viziwi na shule ya sekondari Bashay waliishukuru Taasisi ya Birth Hope Center kwa kuja kuwaletea zawadi za taulo, na kuwaomba waendelee kuwatembelea na siku zijazo.
Msafara huo pia uliongozana na Mheshimiwa Diwani wa viti maalum Tarafa ya Dongobesh, Eliamina Shishi, ambae aliongozana na wataalamu wa Ustawi wa jamii kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Maafisa Habari pamoja na watu wa Birth Hope Center.
Taasisi ya Birth Hope Center wakiwa na Mganga mkuu wa Wilaya Dr.Shadrack Makonda ofisini kwake, Halmashauri ya wilaya ya Mbulu.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.