Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya mbulu Mhe. Michael Semindu Januari 10,2026 wakati wa kikao cha kujadili utekelezaji wa afua za lishe kwa robo ya pili kwa mwaka wa fedha 205/2026.
Mhe. Semindu amewaeleza Watendaji na Wataalamu juu ya namna bora ya utoaji wa elimu ya Lishe kwa wananchi ni kuhakikisha siku ya lishe ya kijiji inafanyika ipasavyo.
“Ili tuweze kufika malengo ya utoaji wa elimu za lishe kwa makundi mbalimbali, watendaji wa kata na vijiji mnao wajibu wa kuhakikisha jamii inapatiwa elimu ya lishe mara kwa mara”, alisema Mhe. Semindu
Aidha, Mhe. Semindu amewaagiza Wataalamu wa Lishe na Elimu kuhakikisha kila shule inaanzisha na kusimamia bustani za mbogamboga ili kuwasaidia wanafunzi kupata lishe bora.
Sambamba na hayo Mhe. Semindu amewasisitiza Watendaji wa Kata na vijiji kusimamia usafi wa mazingira katika maeneo ikiwemo majumbani na shuleni.
Kwaniaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndugu.Damas Debwa ameahidi kuendelea kusimamia kikamilifu utekelezaju wa afua za lishe katika Halmashuauri na kuendelea kuhakikisha watendaji wanasimamia kikamilifu zoezi la usafi wa mazingira.























Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.