Na. Nashon Biseko, Mbulu DC
Kamati ya Siasa Wilaya ya Mbulu kupitia Tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Michael Semindu, Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mhe. Dkt Emmanuel Nuwas, Mbunge kutoka Jimbo la Mbulu Mjini Mhe. Zacharia Isaay, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mhe. Yeconia Maleyecky kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndugu Abubakar Kuuli na Timu ya Watalaamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imetembelea Miradi mbalimbali inayoendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mapema leo tarehe 11.12.2025 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan.
Aidha Timu hii imekagua maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Karatu-Mbulu-Hydom-Sibiti River- Lalago-Maswa wa kiwango cha Lami wenye urefu wa Kilometa 389, Mradi unaendelea vizuri ikiwa kipande cha Mbulu Mji hadi Garbabi chenye urefu wa Kilometa 25 chenye thamani ya Shilingi 36,458,655,171/=Kinaendelea na ujenzi ikitegemewa kukamilika kwa ujenzi huu ifikapo Machi 2026, Ikiwa chanzo cha fedha za Mradi huu ni fedha kutoka Serikali kuu.
Pia Timu hii imekagua Mradi wa Madarasa Mawili na vyoo unaoendelea katika Shule ya Msingi Dongobesh Chini unaolenga kuondoa tatizo la ukosefu wa madarasa ya wanafunzi wenye Mahitaji Maalumu, Ukarabati wa Madarasa 8 na Ofisi 3 ikiwa Mradi huu unathamani ya Shilingi 163,600,000/= ambao chanzo chake ni fedha kutoka Serikali kuu kupitia Program ya BOOST.
Sambamba na Miradi hii timu hii imefika pia katika Ujenzi wa Kituo cha Afya Dinamu – Mamagi ambacho kinahusisha Majengo ya Wagonjwa wa nje, Kichomea taka cha kisasa na Choo cha Wagonjwa wa nje, Mradi huu unagharimu kiasi cha 250,000,000/= hadi kukamilika kwake.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.