Na. Nashon Biseko, Mbuludc
Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mhe. Dkt Emanuel Nuwas amehitimisha kikao chake na Watu wa wenye Mahitaji Maalumu chenye dhamira ya kuimarisha ushirikishwaji na kuinua ustawi wao leo tarehe 24/12/2025, kikao kimefanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Dongobesh na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo Viongozi wa Watu wenye Mahitaji Maalumu kutoka katika ngazi za Mkoa, Wilaya, Kata na Vijiji.
Aidha Dkt Nuwas amesikiliza kero mbalimbali za watu wa mahitaji Maalumu na kuwaahidi kuwapigania katika Nyanja mbalimbali kama Mikopo, Bima kwa wote, ushirikishwaji katika maamuzi, kukusanya mahitaji ya Kundi hili mfano Mawani, Magongo na kuyaweka katika mpango wa utekelezaji.
Sambamba na hayo Dkt Nuwas amesisitiza hatoacha kuwasemea Bungeni wananchi wa Jimbo la Mbulu Vijijini kwa kuhakikisha Serikali inawapa kipaumbele katika mambo mbalimbali ya kimaendeleo kwani Serikali hii ni Sikivu na imejipanga kuwainua Wananchi wake wa makundi yote.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.