Na. Nashon Biseko, Mbulu Dc
Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mhe. Dkt Emanuel Nuwas amepongeza juhudi zinazofanywa na Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi na Timu yake yote katika maendeleo ya miradi na kusisitiza kasi ya ujenzi wa Miradi inayoendelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ili kuendana na makubaliano ya muda uliopangwa kukamilika.
Amesema hayo akiwa katika ziara ya ukaguzi wa Mradi wa Kituo cha Afya kilichopo katika Kijiji cha Gembako, kata ya Masieda tarehe 23/12/2025 akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Michael Semindu, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mhe. Yeconia Maleyecky, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mbulu ndugu Abubakar Kuuli na watalamu mbalimbali kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
Aidha ujenzi wa kituo hiki cha Afya kimehusisha Jengo la Wagonjwa wa nje, Jengo la Upasuaji wa Mama na Mtoto, Jengo la kufulia, Maabara, Choo na Kichomea taka kwa thamani ya shilingi 586,032,142/=
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.