Na Nashon Biseko.
Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mhe. Dkt Emanuel Nuwas leo tarehe 17/12/2025 amefanya Ziara yake ya kwanza kutembelea Shule ya Amali ya Harsha iliyoko kata ya Bashay ili kuona maendeleo ya Ujenzi wa shule hiyo
Akiwa katika ziara hiyo ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndugu Abubakar Kuuli pamoja na timu ya Wataalam wa Halmashauri ya Wilaya, Diwani wa Kata ya Bashay, Wakuu wa Idara, Kamati ya Ujenzi na Uongozi wa Serikali ya Kijiji .
Aidha Dkt. Nuwas amepongeza uongozi wa halmashauri na kijiji kwa usimamizi mzuri wa Ujenzi kwani imekuwa shule bora na ya mfano, pia ametoa wito kwa Serikali kuweza kiasi cha fedha kinachopelea kiweze kutoka ili ukamilishaji wa Ujenzi uweze kukamilika kwa wakati.
Pamoja na shughuli zote kufanyika Dkt Nuwas ameshauri kufanyika mambo mbalimbali ili kuendana na tarehe za ufunguzi kulingana na kalenda ya Serikali pamoja na kufanyika tathimini juu ya ujenzi wa Uzio wa shule. Pia amewaomba wananchi kusaidia kuchimba mifereji ya maji ili kuruhusu ujenzi wa mifumo ya maji katika vyoo na mabweni, kufatilia uunganishwaji wa Umeme kwani miundombinu yake imekamilika, amewaomba mafundi kukamilisha shughuli zilizobaki ili kutoa nafasi kwa wananfunzi wanaoenda kuanza masomo, kufitisha milango iliyo na kufanya marekebisho ya madirisha, pia ametoa ombi la kuwasilisha katika Wizara husika wanafunzi wa kutwa waruhusiwe kujiunga.
Akiongea kwa niaba ya kamati ya Ujenzi pamoja na Serikali ya Kijiji Mhe. Kalisti Diwani wa kata ya Bashay ameishukuru Serikali kwa kuwapangia wanafunzi ili kuanza Masomo yao na ametoa wito kuweza kuongeza Idadi ya Wanafunzi wengine hasa wanaotoka maeneo ya jirani na shule hususani Wilaya ya Mbulu.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.