Wataalamu mbalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Wanasiasa, Wakuu wa Taasisi za Umma na Binafsi, Viongozi wa Dini na Wazee Maarufu wameshiriki Kikao kazi juu ya ufahamu wa Bima ya Afya kwa wote leo 05/01/2026. Kikao kimefunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Michael Semindu na kuongozwa na Watalaamu wa bima ya Afya kutoka Ofisi ya Mkoa wa Manyara.
Bima ya Afya kwa wote ni Bima inayolenga kuwahudumia Wananchi wote bila kujali uwezo wao kiuchumi, bima hii inatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan hivi karibuni ikilenga kuwahudumia Wananchi wote kwa uwiano sawa.
Aidha Bima ya Afya kwa wote ni moja ya sehemu ya ahadi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan aliyoahidi kuitekeleza ndani ya siku 100 endapo atapewa ridhaa ya kuwa Rais katika kampeni za Uchaguzi Mkuu 2025- 2030.
Wanachama wataunda kikundi cha watu 6 na kuchangia kiasi cha shilingi 150,000/= kwa kila kikundi na kwa kila mwaka kama gharama za uendeshaji na kunufaika na huduma ya bima hii, Lakini pia kwa wananchi wasio na uwezo wa kugharamia kiwango hicho Serikali itawagharamia kwa kuhakikisha kila Mwananchi anapata uhakika wa huduma za Afya.
Pia katika kutamatika kwa mafunzo hayo Mhe. Semindu amesisitiza ushiriki wa wananchi katika bima ya afya kwa wote akiwataka washiriki wote wa kikao wakatoe elimu hii katika maeneo yao ili kukamilisha agenda hii muhimu ya uhakika wa huduma ya Afya wote.


Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.