Na. Nashon Biseko, MDC
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Ndugu Michael Semindu Mapema hii leo tarehe 24/11//2025 ametembelea miradi mbalimbali inayoendelea ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu akisisitiza kuongezeka kwa kasi ya ujenzi Pamoja na uwajibikaji kwa Mafundi na wasimamizi wa miradi
Alisema hayo wakati akikagua Miradi mbalimbali ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu akianza na Kituo cha Afya Mamagi – Dinamu kinachoendelea na ujenzi wa Jengo la OPD, Choo cha nje na Kichomea taka wenye thamani ya shilingi 250,000,000 Chanzo cha pesa za mradi huu ni Serikali kuu.
Aidha amekagua mradi wa ujenzi wa shule ya Awali na Msingi unaoendelea ndani ya Shule ya Sekondari Dinamu wenye thamani ya shilingi 330,700,000 ambao upo chini ya Boost, pia amefika katika mradi wa vyoo vya shule ya Msingi Gidhim wenye matundu 19 wenye thamani ya shilingi 49,492,730.74 chini ya SWASH akiwataka Mafundi na wasimamizi wa mradi kuzingatia kasi ili kuendana na kasi ya makubaliano.
Sambamba na miradi hiyo amehitimisha kufanya ukaguzi wa maendeleo ya Mradi wa Shule ya Msingi Dongobesh wa Madarasa ya awali na matundu ya choo chini ya BOOST wenye thamani ya shilingi 163,600,000, Ujenzi wa matundu 7 ya choo katika Shule ya Msingi Mongahay wenye thamani ya shilingi 14,000,000/= na Ujenzi wa madarasa 3 ya shule ya Msingi Endoji madarasa 2 yenye thamani ya shilingi 12,000,000 yakiwa ni Mapato ya ndani na chumba 1 kutoka katika mfuko wa jimbo
Pia DC Semindu amehitimisha ziara yake kwa kuishukuru timu nzima ya ufuatiliaji kutoka katika ofisi ya Halmashauri ya Wilaya kwa ushirikiano mkubwa kwa kuwataka kufuatlia hatua kwa hatua kuhakikisha miradi hii inakamilika kwa wakati.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.