Na Magreth Mbawala,Mbulu DC.
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe. Michael Semindu, leo Novemba 18,2025 ameitaka timu ya wataalamu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kuongeza kasi ya uwajibikaji na utendaji kazi kwenye majukumu ya kila siku ili kuleta ufanisi.
Haya yamesemwa katika kikao kazi kilichofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kikiwa na lengo la kukumbushana na kuwekana sawa kwenye maswala mbalimbali yanayohusu maendeleo.
“Serikali imeleta fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo,wakuu wa Idara na vitengo jukumu lenu ni kusimamia miradi hiyo ikamilike kwa wakati na ubora.”Alisema Mhe. Semindu
Sambamba na hilo Mhe. Semindu aliwataka wakuu wa Idara na Vitengo kuendelea kukusanya mapato na kuzuia mianya ya upotevu wa mapato,kuendelea kupambana na maswala ya ukatili wa kijinsia kwa kutoa Elimu na kuripoti matukio ,kuzingatia usafi wa mazingira na upandaji miti kwenye mazingira yetu na kutoa utaalamu wa maswala ya kilimo kwa sababu tunaelekea kwenye msimu wa kilimo.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbulu Paulo Bura,aliwataka wataalamu kuwa waadilifu na kuzingatia misingi ya utumishi wa umma.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Abubakar Kuuli,alipokea maelekezo na kusema atayafanyia kazi maelekezo yaliyotolewa mara moja .Pia alishukuru kwa kikao kazi hicho chenye tija na kukumbushana maswala mbalimbali ya kiutendaji.
Akifunga kikao kazi hicho,Mhe.Semindu aliwapongeza wataalamu na Halmashauri kwa kufanya vizuri kwenye afua za lishe na pia kwenye maswala ya Elimu.


Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.