Na. Nashon Biseko
Serikali kupitia tume ya Taifa ya umwagiliaji katika kutekeleza ahadi ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuchimba visima virefu vya umwagiliaji kwa ajili ya kuwasaidia wakulima wadogo wadogo wa mazao ya nafaka na mbogamboga imeanza kutekeleza ahadi yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
Mradi huu wa PforR (Program for Result) umezinduliwa mapema hii leo na Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mhe. Dkt. Emmanuel Nuwas katika kata ya Haydom ukihudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ndugu Juma Kilimba, Timu kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu na Timu ya watalamu kutoka Tume ya umwagiliaji ukilenga kuwainua wakulima katika kukuza mapato, kupunguza adha ya upatikanaji wa chakula cha uhakika na kuongeza thamani ya ardhi hasa kwenye maeneo ya mradi bila mkulima kuchangia gharama yoyote pale anapo tumia maji ya mradi huo.
Mradi huu umelenga kila Halmashauri kuchimbiwa visima 5 vyenye urefu zaidi ya Mita 170 ili kuhakikisha upatikanaji wa maji yenye uhakika yatakayotumika mwaka mzima bila upungufu wowote ambapo kata ya Haydom katika Kijiji cha Haydom, Kata ya Maretadu katika Kijiji cha Maretadu chini, Kata ya Masqaroda katika Kijiji cha Masqaroda, Kata ya Dinamu katika Kijiji cha Muslur na Kata ya Dongobesh katika Kijiji cha Qaloda zitanufaika ambapo kila kisima kitakuwa na uwezo wa kumwagilia maji zaidi ya Hekari 40.
Aidha Mhe. Nuwas amawataka wananchi kutumia fursa hii kujiongezea kipato cha uhakika kupitia kilimo na kukuza Uchumi sambamba na kuwataka Wananchi kuwa na utulivu pia kuepuka vurugu zisizo kuwa na tija kwani uwepo wa vurugu huchangia maendeleo kurudi nyuma badala yake kujikita katika shughuli za maendeleo ikiwa kuna changamoto ziwasilishwe katika mamlaka husika na kutatuliwa.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.