Na Nashon Biseko, Mbulu Dc
Katika wiki ya Maadhimisho ya Magonjwa yasiyo ya kuambukiza timu ya Madaktari na Wahudumu wa Afya kutoka Hospitali ya Wilaya ya Mbulu kwa kushirikiana na Wataalamu wa Afya na Lishe kutoka katika Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu wametoa huduma mbalimbali za Afya katika Kijiji cha Lagangesh Mapema hii leo 12.11.2025
Huduma hizi zimetolewa kwa lengo la kuongeza uelewa juu ya umuhimu wa lishe bora, huduma za kitabibu ikiwemo upimaji wa Presha na Sukari sambamba na elimu ya kujikinga na Magonjwa yasiyo ya kuambukiza pamoja na elimu ya huduma rafiki kwa vijana.
Pia huduma hii imelenga kuwakwamua wanakijiji dhidi ya Magonjwa mbalimbali yasiyo ya kuambukiza na yatokanayo na ukosefu wa lishe bora, Umuhimu wa Uzazi wa Mpango, Umuhimu wa Kliniki kwa Wajawazito na Umuhimu wa kujifungulia katika vituo vya Afya.
Aidha watalamu wa Lishe wameshauri kuzingatia Makundi 6 ya Vyakula kama Vyakula asili vya nafaka, mizizi na ndizi mbichi, Vyakula asili ya Wanyama, Vyakula jamii ya mikunde na m,begu za mafuta, Mbogamboga, Matunda pamoja na Mafuta, Sukari, Asali na Chumvi wakiwashauri wanakijiji kuwa unachokula ndicho kinaamua Afya yako mfano matumizi mabaya ya mafuta, chumvi, sukari, pombe na sigara yanauwezo mkubwa wa kukuletea magonjwa badala yake kuzingatia makundi 6 ya chakula kwa lengo la kujenga afya kwani Magonjwa hayachagui Mtoto, Kijana au Mzee.
Baada ya huduma hizo Watoto wameandaliwa uji wa lishe pamoja na kufanyiwa tathimini ya hali ya lishe sambamba na kupewa Matone ya Vitamin A na dawa za Minyoo.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.