Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imepokea tuzo za pongezi kwenye kikao cha tathmini ya lishe ya Mkoa kilichofanyika 12/09/2025 katika ukumbi wa vikao kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Tuzo hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imeshika nafasi ya kwanza(1) kati ya Halmashauri saba Kimkoa kwenye usimamizi mzuri na upatikanaji wa bidhaa za afya.Pia Halmashauri imeingia kwenye kumi bora ya waliofanya vizuri Kitaifa kati ya Halmashauri 184 nchini.
Pia Halmashauri imepokea tuzo ya mshindi wa pili(2) kimkoa kwa sababu ya utekelezaji wa mkataba wa lishe,ikiwa na asilimia 99.4.
Mwisho Halmashauri ilipongezwa kwa kuongeza mapato katika kituo cha Afya Dongobesh kutoka Milioni 3 hadi kufikia Milioni 18 kwa Mwezi.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.