• Mlalamikaji |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Mbulu District Council
Mbulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Taasisi
    • Orodha ya Wakurugenzi
  • Utawala
    • Idara
      • Idara ya utumishi na mahusiano
      • Mipango, Takwimu na Uangalizi
      • Idara ya Fedha
      • Elimu na Utamaduni
      • Afya
      • Kilimo.Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na uthibiti wa taka ngumu
      • Uvuvi na Ufugaji
      • Idara ya Ujenzi na Zimamotto
        • Moto
      • Idara ya Maji
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Goverment Communication
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Miongozo
    • Sheria
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Picha Jongefu
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
  • Miradi
    • Miradi iliyopitishwa
    • Miradi inayoendela
    • Miradi iliyokamilika
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Dinamu
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Uchumi
      • Kamati ya Ardhi
      • Kamati ya ALAT
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba za Vikao
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Sekta ya Viwanda
    • Sekta ya Kilimo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Elimu

Jafo asema Uchaguzi Serikali za Mitaa uko pale pale, Novemba 24, 2019

Kurushwa hewani: November 9th, 2019

Imewekwa Tar: November 9th, 2019

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesema Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uko pale pale na utafanyika Novemba 24, 2019 kama ilivyopangwa licha ya vyama vingine kujitoa kwenye Uchaguzi huo.

Jafo ameyasema hayo mapema leo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari Ofisini kwake Jijini Dodoma kuhusu maendeleo ya  maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa ya zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kugombea uongozi sambamba  na Kamati za Rufaa.

Alisema zoezi la uchukuaji wa urejeshaji wa fomu za kugombea uongozi limeenda vizuri na wananchi waliochukua fomu ni 555,036 na waliorejesha ni 539,993 sawa na asilimia 97.29 ya wananchi wote waliochukua fomu, na ambao hakurejesha ni asilimi 2.7 tu.

“Hii inaonyesha muamko mkubwa wa wananchi kutaka kuongoza katika ngazi ya Serikali za Mitaa na mchakato mzima wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu ulienda vizuri ukiwa na Kanuni bora zaidi  kulinganisha na chaguzi zilizotangulia” alisema Jafo.

Aliongeza kuwa baada ya zoezi hili kukamilika lilifuatiwa na uteuzi ambao ulilenga kuteua wagombea wenye sifa, waliokidhi vigezo na kufuata taratibu zote za ujazaji wa fomu za kugombea na kubandiwa kwa orodha ya wagombea waliopitishwa katika hatua hiyo.

Wagombea pia walipata fursa ya kuwasilisha pingamizi zao kwa mujibu wa Kanuni na kisha kukata rufaa kwenye Kamati ya Rufaa za Wilaya zilizoundwa kwa ajili ya kuratibu rufaa za wagombea alisema Jafo.


Waziri Jafo alifafanua kuwa mpaka hivi sasa rufaa zilizowasilishwa kutoka kwenye vyama mbalimbali vya siasa ni 13,500 na zinafanyiwa kazi na Kamati za Rufaa za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo zoezi hilo litakamilika leo hii Tarehe 09/11/2019.

Akizungumzia baadhi ya vyama kujitoa kwenye Uchaguzi ilihali wanachama wao walishateuliwa amma kuwasilisha rufaa zao kwenye Kamati  alisema kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi jina la mgombea likishateuliwa linabaki kwenye karatasi za kupigia kura siku ya Tarehe 24/11/2019 hata kama chama chake kimejiungea kushiriki kwenye Uchaguzi .

Aliendelea kuelezea kuwa wakati zoezi la uteuzi na kamati za rufaa zikiendelea na kazi yake alipata fursa ya kufanya ziara katika mikoa ya Singida, Manyara, Dododma,Iringa na Njombe ambapo  alijionea baadhi ya makosa yaliyofanywa na wagombea wakati wa ujazaji wa fomu lakini pia alizungumza na Kamati za Rufaa.

Alitaja makosa yaliyobainishwa kwenye fomu za wagombea kuwa ni  “Kujaza umri mdogo kuliko umri unaostahili kwa mgombea, sehemu ya tarehe kuweka sahihi au mtu kuchukua fomu na kujidhamini mwenyewe au majina kutofautiana wakati wa kujiandikisha kwenye orodha ya mpigakura na kwenye fomu ya kugombea hivyo Wasimamizi walifanya kazi yao kwa mujibu wa miongozo na Kanuni za Uchaguzi” Alisema Jafo.

Lakini bado nafasi ilikuwepo endapo mgombea  angeona hakuteuliwa kwa kuonewa ipo Kamati ya Rufaa ambayo ingeweza kuskiliza malalamiko ya mgombea na kuyafanyia kazi alisisitiza Jafo.

“Kuanzia kesho tutaanza kutoa Taarifa ya Rufaa zilizopita na watu walioteuliwa kushiriki uchaguzi huo kupitia Kamati za Rufaa alimalizia Waziri Jafo.


Matangazo

  • Tangazo la fursa za mafunzo ya ufundi stadi awamu ya saba February 01, 2025
  • TANGAZO LA ZABUNI YA UCHIMBAJI VISIMA January 29, 2019
  • JINSI YA KUTOA/KUTUMA MALALAMIKO KWA NJIA YA MTANDO HALMSHAURI YA WILAYA YA MBULU. March 23, 2019
  • KARIBU MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU 2021 June 10, 2021
  • Tazama zote

Habari za hivi Punde

  • MBULU DC YATOA SADAKA KITUO CHA AFYA DONGOBESH.

    January 30, 2025
  • MBULU DC YAKWAMUA VIKUNDI VYA VIJANA KIUCHUMI

    February 13, 2025
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA BAJETI YA BILIONI 38.7 KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026

    February 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI LAHIMIZA WANAFUNZI WARIPOTI SHULENI

    January 31, 2025
  • Tazama zote

Picha Jongefu

MBULU DC KUKUSANYA ZAIDI YA MIL.90 KATIKA MSIMU MPYA WA UVUVI KUTOKA BWAWA LA BONDELA YAEDA CHINI
Video za Ziada

Viunganishi ya Haraka

  • Facility Financial Accounting and Reporting System(FFARS)
  • Log in PlanRep System
  • PlanRep Documents
  • FFARS USER GUIDE
  • MANYARA REGIONAL WEBSITE
  • UTUMISHI PORTAL

link tunazolandana

  • TOVUTI YA IKULU
  • MFUMO WA VIBALI YA KUSAFIRI NJE (LIVE)
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA TAMISEMI
  • BARAZA LA MTIHANI LA TAIFA TANZANIA
  • TOVUTI YA HABARI MAELEZO

Watembeleaji wa Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Uelekeo wa Ramani

Wasiliana nasi

    Mbulu district Coucil

    Anuani: P.O.BOX 74

    Simu ya mezani: +255743583078

    Simu: +255716992222

    Barua pepe: md@mbuludc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Awali
    • Kanusho
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.