Na, Ruth Kyelula.
Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Lutengano Emmanuel amesema kuwa kwa kipindi cha mwezi July mpaka September watoto wenye utapiamlo mkali waliolazwa walikuwa kumi na wote walipatiwa matibabu na kurudi nyumbani na wazazi wao kupewa unasihi namna ya kuandaa lishe bora kwa ajili ya watoto hao ili waweze kupona utapiamlo na kurejea kwenye hali yao ya kawaida.
Afisa Lishe Lutengano Emmanuel akieleza kamati shughuli mbalimbali za lishe.
Hayo yalisemwa na Afisa lishe wakati wa kikao cha kamati ya lishe cha robo ya kwanza, kikielezea kazi mbalimbali zilizofanywa na Maafisa lishe kwa kipindi cha mwezi July hadi September, 2024.Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Halmashauri Octoba 24,2024.
Afisa Lishe wa Willaya Jackline David (wa kwanza kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Juma Kilimba (wa kwanza kulia) wakifuatilia kwa makini wasilisho la Afisa Lishe.
“Miongoni mwa shughuli zilizotekezwa ni pamoja na uchunguzi wa hali ya lishe ambapo jumla ya watoto elfu moja mia moja arobaini na tisa (1149) waliolazwa wodini kumi walikuwa na utapiamlo mkali ambao ni sawa na asilimia 0.008 na saba waliokuwa na utapiamlo wa kadri ni asilimia 0.006 na waliokutwa na ukondefu ni asilimia 0.1, ambao ni watoto mia moja kumi nanne (114) kati ya elfu moja mia moja arobaini na tisa (1149). Lakini pia matibabu yalifanyika wodini kwa watoto wenye utapiamlo mkali.” Alisema Lutengano.
Wajumbe wa kamati ya lishe wakisikiliza repoti ya shughuli za lishe kwa mwezi July mpaka Septemba.
Aliendelea kusema kuwa, mbali na hilo waliweza kutoa matone ya vitamini A, ambapo jumla ya watoto elfu thelathini na tisa mia saba themanini na sita (39786) sawa na asilimia mia waliweza kuhudumiwa.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.