Na, Ruth Kyelula, Mbulu - DC.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbulu, Paulo Bura ambae amemuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, amewataka Watendaji wa Kata, wazingatie maadhimisho ya siku za Lishe katika vijiji vilivyomo katika Kata zao ili kuweza kuleta tija katika kutekeleza afua za Lishe na jamii iweze kupata elimu juu ya umuhimu wa Lishe bora katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
Katibu Tawala wa Wilaya, Paulo Bura akizunguza na wajumbe wa kikao cha Lishe.
Hayo yalisemwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbulu, Paulo Bura, wakati wa ufunguzi wa kikao cha Lishe cha robo ya kwanza ya 2024/25 katika ukumbi wa Halmashauri Desemba 18, 2024.Ambapo Watendaji wa Kata na baadhi ya Wataalamu walishiriki kikao hicho.
Aidha Katibu Tawala ameiomba ofisi ya Mkurugenzi kukamilisha asilimia ya fedha za Lishe ambapo mpaka sasa imetolewa asilimia 80.81. Ahakikishe inafika asilimia 100.Ili Halmashauri iweze kupanda katika shughuli zake za Lishe.
Watendaji wa Kata wakifuatilia kikao cha Lishe cha robo ya kwanza.
“Januari tufanye kikao mapema, ili tuone mwajiri kwenye kipengele cha fedha ametoa? wale wenye nyekundu wameondoa? naomba kama ulikua hujaingia kwenye nyekundu usiingie, ninachosisisitiza hapa jambo hili liwe sehemu ya maisha yetu ya kila siku, tufuatilie kama tunavyofuatilia ratiba za vitu vingine.” Alisema Bura.
Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Joseph Sambo amesema kuwa wamepokea maelekezo na wataenda kuyafanyia kazi kikamilifu ikiwemo na utengaji wa fedha katika robo ya kwanza zifike asilimia mia moja kwa shughuli za Lishe.
Naye Afisa Lishe wa Wilaya Jackline David, ameomba walezi wa Kata na Watendaji wa Kata wasimamie Kata zao ili kila robo vijiji vyote viweze kufanya maadhimisho ya siku za Lishe.Ili elimu ya Lishe, Afya na mambo ya chanjo inaifikia jamii kwa ukubwa.
Afisa Lishe wa Wilaya, Jackline David akiwasilisha shughuli mbalimbali za Lishe zilizofanyika kwa kipindi cha robo ya kwanza.
Aidha Afisa Lishe wa Wilaya ametoa wito kwa walezi wa Kata, Watendaji wa Kata na Vijiji washirikiane katika masuala mazima ya Lishe katika jamii zinazotuzunguka.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.