Na Magreth Mbawala, Mbulu DC.
Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari kuhusu ugonjwa wa UKIMWI kwa kujikinga na ngono zembe,kupima afya na kutumia dawa za ARV kikamilifu mara watakapogundulika ni wagonjwa.
Hayo yamesemwa leo Disemba 1,2025 na Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Neema Aligawesa akiwa amemwakilisha Mbunge wa Mbulu Vijijini Mhe. Dr. Emanuel Nuwas ikiwa ni siku ya Maadhimisho ya UKIMWI duniani iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Gidhim.
“UKIMWI bado upo hivyo ni vema kila mmoja aendelee kuchukua tahadhari,tujikinge na tuwakinge tuwapendao.”Alisema Aligawesa
Sambamba na hilo huduma mbalimbali zilitolewa ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi, upimaji wa Afya (VVU), huduma za uzazi wa mpango na huduma za kuchunguza hali ya lishe.Waliochunguzwa VVU ni watu 103,Wanawake71 na Wanaume 32 kati yao hakuna aliyepatikana na VVU.
Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Dr.Shadrack Makonda aliwashukuru waandaaji ,taasisi mbalimbali ,vikundi vya sanaa na ngoma pamoja na Wananchi wa kata ya Gidhim kwa kujitokeza kwa wingi kwenye maadhimisho hayo.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani kwa mwaka 2025 ni “Imarisha mwitikio-tokomeza UKIMWI”
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.