Na Magreth Mbawala, Mbulu DC.
Wanamichezo Maria John Tarmo na Mariam Elikana Gadie jana tarehe 03/12/2025 wamepokelewa kwa shangwe kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mara baada ya kurejea kutoka kwenye Mashindano ya kitaifa ya wanawake ya mchezo wa riadha.
Maria John Tarmo alishinda mshindi wa tatu kwenye mashindano ya kurusha mkuki kitaifa na mwakani 2026 anatarajia kwenda nchini Japan kuwakilisha nchi kimataifa.Huku Mariam Gadie akiwa ameshika nafasi ya tano kwenye riadha na kupelekea kupata ufadhili wa masomo katika Shule ya Sekondari Filbert Bayi iliyopo Mkoani Pwani.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mhe.Yeconia Maleyecky aliwapongeza sana kwa kufanya vizuri na kuwataka madiwani waibue vipaji kutoka kwenye kata zao.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Abubakar Kuuli aliwapongeza wanamichezo hao na kuwataka waendelee na mazoezi ili waendelee kufanya vizuri.Pia aliwaambia wakiwa na changamoto yoyote wasisite kufanya mawasiliano nae.
Aidha,Mbunge wa Mbulu Vijijini Mhe.Emanuel Nuwas,aliwapongeza wanamichezo hao kwa kuitangaza Mbulu Vijijini vizuri na kuwataka Maafisa michezo wa Halmashauri kuendelea kuibua vipaji zaidi.
Mwisho madiwani waliwapongeza wanamichezo kwa kufanya vizuri na kuahidi kuongeza bajeti katika eneo la michezo ili kuendelea kupata vipaji zaidi.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.