• Mlalamikaji |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Mbulu District Council
Mbulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Taasisi
    • Orodha ya Wakurugenzi
  • Utawala
    • Idara
      • Idara ya utumishi na mahusiano
      • Mipango, Takwimu na Uangalizi
      • Idara ya Fedha
      • Elimu na Utamaduni
      • Afya
      • Kilimo.Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na uthibiti wa taka ngumu
      • Uvuvi na Ufugaji
      • Idara ya Ujenzi na Zimamotto
        • Moto
      • Idara ya Maji
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Goverment Communication
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Miongozo
    • Sheria
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Picha Jongefu
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
  • Miradi
    • Miradi iliyopitishwa
    • Miradi inayoendela
    • Miradi iliyokamilika
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Dinamu
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Uchumi
      • Kamati ya Ardhi
      • Kamati ya ALAT
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba za Vikao
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Sekta ya Viwanda
    • Sekta ya Kilimo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Elimu

Kampeni ya Uhamasishaji Chanjo ya UVIKO 19 Yazaa Matunda Kwa 86.3% ya Chanjo Hiyo Imetumika Hadi 14.10.2021

Kurushwa hewani: October 17th, 2021

Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Sezaria V. Makota Katika Uhamasishaji Kata ya Maretadu na Kulia ni Katibu Tawala Wilaya ya Mbulu Bi. Sara Sanga.




Kaimu Mganga Mkuu Dr. Shirima Katika Uhamasishaji Kata ya Maretadu.


Nyenzo za Uhamasishaji Zinawekwa Sawa Kwa Kuongeza Mafuta Kwenye Jenereta, Kata ya Eshkesh.



Bw. Edes Malley wa Kitengo cha Matangazo Katika Kamati Hii ya Wilaya ya Uhamasishaji UVIKO 19, Kata ya Eshkesh.


Zoezi la Uchanjaji Likiendelea Baada ya Uhamasishaji wa UVIKO 19 kueleweka, Kata ya Eshkesh.


Baada ya Kazi Hapa ni Masuala ya Chakula Huko Huko Porini, Kata ya Eshkesh.


Kamati ya Uhamasishaji UVIKO 19, Kata ya Endamilay.



Zoezi la Uhamasishaji UVIKO 19 Likiendelea, Kata ya Endamilay.


Wananchi Wakiuliza Maswali Katika Mkutano Huo wa Uhamasishaji UVIKO 19, Kata ya Endamilay.

Kamati ya Wilaya ya Uhamasishaji UVIKO 19, Wakiwa Kata ya Endamilay.Padri Kanisa la Roma Gidhim.


Zoezi la Uhamasishaji Likiendelea Ndani ya Kanisa la Roma Baada ya Kupata Idhini ya Padri.

Waumini wa Kanisa Hilo.


Zoezi la Uchanjaji Lilinaendelea Baada ya Uhamasishaji wa UVIKO 19 Kueleweka, Kanisa la Gidhimi na Roma Dongobesh.


Zoezi la Uhamasishaji wa UVIKO 19 Likiendelea Katika Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Eshkesh.









~~~~~~~~~~    HABARI KWA UNDANI ZAIDI    ~~~~~~~~~~




Mafanikio haya yamepatikana kwa ushirikiano wa dhati toka kwa Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Sezaria V. Makota ambaye alifungua kampeni hii tarehe 30.09.2021 Kata ya Maretadu ambapo takribani watu wapatao 50 walichanjwa katika kampeni hiyo pale pale na kuendelea katika maeneo mengine kwa wilaya nzima kwa msisimko ule ule.

Hadi tarehe 13/10/2021 Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu imechanja jumla ya watu 1447 kati ya dozi 1675 na kubaki 25 tu. Awali kama Wilaya ilipokea chanjo aina ya "Jansen n Jansen" ya Marekani dozi 2000 lakini dozi 325 zilichukuliwa na Hospitali ya Mkoa kwenda kutumika huko baada ya mahitaji kuwa mengi zaidi ya dozi walizonazo na hili ni jambo la kawaida kwa utendaji kazi wa afya kote nchini, lakini dozi 205 ziliharibika kutokana na sababu mbalimbali.

Katika  hali ya kuhakikisha wananchi wote wanaendelea kufanya kazi zao vizuri kiuchumi, kijamii, ndani na nje ya nchi hatimaye kuwa salama na gonjwa hatari la UVIKO 19 Mh. Mkuu wa Wilaya  alihamasisha kwa nguvu zote, kijiji kwa kijiji kata hadi kata ili tu elimu iwafikie itakayopelekea wananchi kuwa na mwamko wa kuchanja UVIKO 19 bila shida. Kisha timu ya Wilaya ya UVIKO 19 iliyopata mafunzo kimkoa iliendelea na kampeni ya uhamasishaji kwa  kasi katika maeneo  yenye watu wengi, kwenye matukio na popote ambapo pana shuguli za kiuchumi na kijamii kuanzia viwanja vya mpira, stendi za mabasi, sokoni, mitaa ya biashara na vijiji hadi kwa wavuvi Yaeda chini na Eshkesh.

Imefahamika kutoka kwa Wataalamu wa afya kwamba hakuna madhala wakati na baada ya kuchanja kama inavyosemekana na wengi kwani cha kwanza kabisa hutaweza kuambukizwa tena na UVIKO 19 na ikitokea ukapata basi hutaathirika kwani kinga zitakuwa zimeimarika sana kutokana na mwili kujijengea kinga ya awali iliyotengenezwa kutokana na chanjo iliyoko mwilini, wakati huo huo ambaye hajachanjwa akiambukizwa anakuwa hana kinga ya kutosha lakini mbaya zaidi hutumia gharama kubwa sana katika kujitibu ambapo kwa utafiti uliofanywa  na wataalamu wa afya nchini Tanzania imejulikana kwamba ni kati ya Tsh. 200,000 hadi Tsh. 300,000 kwa siku gharama za kuokoa uhai wa mgonjwa wa UVIKO 19 kwa kununua mitungi ya kuongeza heya ya "Oxygen" tu, hivyo wananchi wanatakiwa kufanya juu chini kuchanja, kwasababu ndiyo kinga pekee hadi sasa kwani hakuna dawa ila watabibu wote hutibu dalili inayojitokeza kwa mgojwa; mfano kama anaharisha atatibiwa kuhara ili asiendelee kuharisha.

Maswali yanayoulizwa mengi ni kwamba binadamu baada ya kuchanjwa atapata ugumba jambo ambalo sio kweli wanaume kwa wanawake wanaendelea na uzazi wao kama kawaida, juu ya suala wajawazito na wanaonyonyesha imefahamika kwamba hayo ndiyo makundi yaliyo hatarishi zaidi kwani kinga zao zinakuwa zipo chini kutokana na hali aliyonayo hivyo yeye anapaswa achanje na haina madhara kwa mama na mtoto aliyepo tumboni au anayenyonya pia.

Kuna wanaouliza kwamba hubadilisha vinasaba vya binadamu yaani "DNA" hiyo si kweli kwani chanjo yoyote ili ibadilishe Vinasaba "DNA" basi ni lazima iingie kwene kiini cha seli husika ambayo kitaalamu inaitwa "Neuclear" ambapo chanjo hizi haziingii kwene kiini cha seli bali hufanya kazi sehemu ya nje tu na haina kiwezeshi chochote cha protini cha kuifanya iingie ndani ya kiini "Neuclear" na kukaa humo.

Pia wapo wanaouliza kwa nini imefanyika kwa haraka haraka hivi ukilinganisha na chanjo zingine zinachukua hadi miaka 10 ndipo ianze kutumika kwa mwanadamu? katika kujibu hili ni kwamba huu ugonjwa wa mafua unaotokana na kirusi haujaanza leo kwasababu kwa takwimu zilizopo duniani ulikuwepo mwaka 2002 ugonjwa wa mafua ujulikanao kama "SARS" na kisha ukafuata "MARS" huko uarabuni uliua sana watu, yakaja mafua ya ndege, na baadaye mafua ya nguruwe na mengine mengi ambapo mwanadamu katika kukabiliana na hili alishaanza utafiti kupitia Shirika la Afya Duniani "WHO" na taasisi zingine mbalimbali za kimataifa lakini kwakuwa magonjwa haya yalikuja kutoweka yenyewe basi ikawa tafiti zote za kisayansi kutoendelea na kukoma baada ya dunia kuwa salama. 


Hivyo baada ya huu ugonjwa wa UVIKO 19 kuonekana tena watafiti wale wale wakaanzia pale pale walipoishia na utafiti wa awali kiasi cha kupelekea kupata majibu mapema. Jingine ni kwamba kwa sasa utaalamu wa kibinadamu katika kuchambua mambo umeongezeka tofauti na miongo 3 iliyopita, vifaa na teknolojia ya kitabibu navyo vimeongezeka kwa kiwango cha ajabu kabisa jamba ambalo ukokotoaji wa data za sampuli za kitu chochote hutumia muda mfupi kutokana na vifaa tehama vya sasa kuwa vya kisasa zaidi na vya kimamboleo kwa maana ya uwezo wa hali ya juu sana. Mfano hai ni hesabu iliyokuwa inafanywa siku 3 kwa kompyuta ya miaka ya 1950 kwa sasa inatumia sekunde tu kufanya kitu kile kile, sababu nyingine ni kwamba ugonjwa wa UVIKO 19 unasambaa kwa haraka kwa watu wengi na pia humuua mgojwa kwa haraka sana ambapo kitabibu imesaidia kumfuatilia mdudu husika yaani kirusi namna anavyoathili mwili na hivyo kupata majibu ya mapema ya mzunguko wa majaribio ya dawa husika kwa haraka ukilinganisha na magonjwa mengine ya chanjo yanayochukua muda mrefu hadi mtu kuathirika vibaya.

Kwa nini tuiteue "Jansen n Jansen" ya Marekani, ni kwamba ndiyo chanjo inayoweza kuhifadhika kwa mazingira yetu hadi vijijini kulingana na vifaa tulivyonavyo yaani nyuzi joto la 2C hadi 8C tofauti na zingine zenye hadi nyuzi joto hasi -50C, lakini pia ndiyo chanjo ya kwanza kuifanyia uchunguzi kwa madaktari bingwa wa Tanzania katika kituo cha utafiti kilichopo Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine "SUA"


Kama ni kupata homa au maumivu kiasi kwa siku 2 au 3 za mwanzo ni kwa baadhi ya watu lakini ndiyo kawaida ya dawa yoyote ambayo huwa ngeni mwilini mwako kama ilivyo chanjo zingine pamoja na madawa mengine ya magonjwa ya maralia, "typhoid" na mengine mengi kwamba ukisha kunywa tu basi mwili katika kupokea dawa hizi utajiskia hali fulani lakini haimaanishi haitakutibu malalia au "typhoid" uliyonayo, mbona klorokwini za homa kwa kipindi fulani hivi watu walikuwa wanawasha sana na pia "Metachelfine" inakunyong'onyesha kabisa na mwili kulegea lakini huwa ndio kupona kwenyewe.

Hata hiyo kama Rais wetu Mhe. Samia S. Hassan amechanjwa na Mawazili, Wakuu wa Mikoa na Wilaya, Wakurugenzi, Wakuu wa Idara na Vitengo, wataalamu wa afya, Mameneja na Wakuu wa taasisi zote za serikali wamechanjwa hii inaonyesha namna gani inavyoaminika kuwa ni salama na kwako pia.

Vituo vya kuchanjia ni sehemu zote za kutolea huduma ya afya kuanzia Zahanati, Vituo vya afya na Zospitali zote za Wilaya huku gali la kliniki linayotembea hutoa pia huduma hiyo popote linapokuwa linatembea ili kumrahisishia mwananchi kupata huduma kwa haraka vijijini, lakini hata kama wewe ni mwananchi na mkazi wa Mbulu wilaya uko Dar es salaam, Mwanza au mbeya au popote unaruhusiwa kwenda kituo chochote cha kutolea huduma ya afya kilicho karibu nawe utapa chanjo hii na usaidizi wa maelekezo mengine ya Daktari. 

Serikali itaendelea kupokea aina zingine za chanjo zitakazothibitishwa na madaktari wetu bingwa wa hapa nchini kama vile chanjo ya "Sinopharm" ya China na sisi hatuwezi kukaa kama kisiwa kwani nchi zote zinautaratibu huu duniani wa kuchanja chanjo hii hii.










Matangazo

  • Tangazo la fursa za mafunzo ya ufundi stadi awamu ya saba February 01, 2025
  • TANGAZO LA ZABUNI YA UCHIMBAJI VISIMA January 29, 2019
  • JINSI YA KUTOA/KUTUMA MALALAMIKO KWA NJIA YA MTANDO HALMSHAURI YA WILAYA YA MBULU. March 23, 2019
  • KARIBU MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU 2021 June 10, 2021
  • Tazama zote

Habari za hivi Punde

  • MBULU DC YATOA SADAKA KITUO CHA AFYA DONGOBESH.

    January 30, 2025
  • MBULU DC YAKWAMUA VIKUNDI VYA VIJANA KIUCHUMI

    February 13, 2025
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA BAJETI YA BILIONI 38.7 KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026

    February 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI LAHIMIZA WANAFUNZI WARIPOTI SHULENI

    January 31, 2025
  • Tazama zote

Picha Jongefu

MBULU DC KUKUSANYA ZAIDI YA MIL.90 KATIKA MSIMU MPYA WA UVUVI KUTOKA BWAWA LA BONDELA YAEDA CHINI
Video za Ziada

Viunganishi ya Haraka

  • Facility Financial Accounting and Reporting System(FFARS)
  • Log in PlanRep System
  • PlanRep Documents
  • FFARS USER GUIDE
  • MANYARA REGIONAL WEBSITE
  • UTUMISHI PORTAL

link tunazolandana

  • TOVUTI YA IKULU
  • MFUMO WA VIBALI YA KUSAFIRI NJE (LIVE)
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA TAMISEMI
  • BARAZA LA MTIHANI LA TAIFA TANZANIA
  • TOVUTI YA HABARI MAELEZO

Watembeleaji wa Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Uelekeo wa Ramani

Wasiliana nasi

    Mbulu district Coucil

    Anuani: P.O.BOX 74

    Simu ya mezani: +255743583078

    Simu: +255716992222

    Barua pepe: md@mbuludc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Awali
    • Kanusho
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.