• Mlalamikaji |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Mbulu District Council
Mbulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Taasisi
    • Orodha ya Wakurugenzi
  • Utawala
    • Idara
      • Idara ya utumishi na mahusiano
      • Mipango, Takwimu na Uangalizi
      • Idara ya Fedha
      • Elimu na Utamaduni
      • Afya
      • Kilimo.Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na uthibiti wa taka ngumu
      • Uvuvi na Ufugaji
      • Idara ya Ujenzi na Zimamotto
        • Moto
      • Idara ya Maji
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Goverment Communication
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Miongozo
    • Sheria
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Picha Jongefu
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
  • Miradi
    • Miradi iliyopitishwa
    • Miradi inayoendela
    • Miradi iliyokamilika
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Dinamu
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Uchumi
      • Kamati ya Ardhi
      • Kamati ya ALAT
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba za Vikao
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Sekta ya Viwanda
    • Sekta ya Kilimo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Elimu

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamduni,Sanaa na Michezo amtembelea mwanariadha anayeheshimika duniani Mzee John Steven- Mbulu

Kurushwa hewani: May 21st, 2018

Na mwandishi: Komanya May 22, 2018

1

 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akisalimiana na Mzee John Steven Akhwari  Mwanariadha anayeheshimika Duniani mara baada kwasili alipomtembelea nyumbani kwake Eneo la Sanubaray mjini Mbulu  mkoani Manyara jana, John Steven Akhwari aliiwakilisha nchi katika michezo ya Olimpiki iliyofanyika Mexco  City mwaka 1968

John Steven Akwari aliyekuwa wa mwisho kumaliza mashindano ya marathon mwaka 1968 Mexico City katika mioyo ya mamilioni ya watu anakumbukwa kama shujaa ambapo mwaka 2008 katika mashindano ya Olimpiki ya Beijing nchini China miaka 40 baadaye, Akhwari aliteuliwa kuwa balozi wa heshima wa Olimpiki. Katika mashindano hayo ya mwaka 1968, Akwari akiwa na umri wa miaka 30 akiiwakilisha Tanzania alikuwa mwanariadha wa mwisho (57) kumaliza mashindano kati ya 75 walioanza.

 

Mshindi wa mashindano hayo Mamo Wolde wa Ethiopia alitumia saa 2:20:26 huku Akhwari akimaliza zaidi ya saa moja baadaye yaani alitumia saa 3:25:27 kukiwa na watazamaji wachache uwanjani na jua lilikwisha kuzama. Awali wakati anaanza mbio hizo, Akwari alianguka na kupata majeraha kwenye goti ikichangiwa kwa kiasi kikubwa na hali ya hewa ya Amerika ya kati kuwa tofauti na nyumbani. Wanariadha wenzake walimpita moja baada ya mwingine na hivyo kukatiza ndoto yake ya kuiletea Tanzania medali ya kwanza kabisa ya Olimpiki, lakini hakukata tamaa bali alinuia kumaliza hayo mashindano.

 

Akiwa amefungwa bandeji mguuni huku akitokwa na damu, Akhwari alitokeza uwanjani saa moja baada ya mshindi kutangazwa, na kukiwa na watazamaji wachache na waandishi wa habari na giza likianza kuingia, uwanja ulizizima kuona Akhwari anachechemea akiwa na maumivu kuelekea mstari wa kumaliza mbio, wengi waliguswa baada ya kushuhudia tukio hilo. Alipoulizwa na waandishi kwa nini aliendelea na mashindano baada ya kuumia, aliwajibu kwa utulivu jibu rahisi “Nchi yangu haikunituma maili zaidi ya 5000 kuanza mbio, bali kuzimaliza“

2    3

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga akisalimiana na MZee John Steven Akhwari wakati alipoongozana na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo aliyemtembelea mzee huyo nyumbani kwake eneo la Sani mjini Mbulu.

5

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akizungumza jambo na Mzee John Steven Akhwari.

6

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akimsikiliza Mee John Steven Akhwari alipokuwa aktoa maelezo kwake kuhusu mbambo mbalimbali aliyowahi kuyafanya katika masuala ya mchezo wa Riadha.

7

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu wakiangalia tuzo mbalimbali ambazo Mzee John Steven Akhwari kulia aliwahi kutumikiwa.

8


 10

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu wakionyeshwa mwenge wa Olimpiki ambao  Mzee John Steven Akhwari kulia  kutumikiwa jijini Beijing China baada ya kuukimbiza akiwa Balozi wa Mashindano hayo mwaka 2008.

11

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi  akionyeshwa moja ya tuzo  ambayo Mzee John Steven Akhwari alitunukiwa nchini Uswisi .

12

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi  akionyesswa Nisahani ambayo Mzee John Steven Akhwari alitunukiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi

13

Hapa wakionyeshwa vyeti mbalimbali ambavyo Mzee John Steven Akhwari aliwahi kutunikiwa kutambua mchango wake katika mchezo wa Riadha.

14

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga wakiwa katika picha ya pamoja na Mzee John Steven Akhwari mara baada ya mazungumza yao.



Matangazo

  • Tangazo la fursa za mafunzo ya ufundi stadi awamu ya saba February 01, 2025
  • TANGAZO LA ZABUNI YA UCHIMBAJI VISIMA January 29, 2019
  • JINSI YA KUTOA/KUTUMA MALALAMIKO KWA NJIA YA MTANDO HALMSHAURI YA WILAYA YA MBULU. March 23, 2019
  • KARIBU MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU 2021 June 10, 2021
  • Tazama zote

Habari za hivi Punde

  • MBULU DC YAADHIMISHA SIKU YA WAUGUZI DUNIANI.

    May 16, 2025
  • KAMATI LISHE YAKAA KIKAO CHA TATHIMINI YA HALI YA LISHE KWA ROBO YA TATU

    May 08, 2025
  • MADIWANI WAPONGEZWA KWA USIMAMIZI MZURI WA MIRADI KATIKA KATA ZAO

    April 29, 2025
  • MBULU DC YATOA SADAKA KITUO CHA AFYA DONGOBESH.

    January 30, 2025
  • Tazama zote

Picha Jongefu

MBULU DC KUKUSANYA ZAIDI YA MIL.90 KATIKA MSIMU MPYA WA UVUVI KUTOKA BWAWA LA BONDELA YAEDA CHINI
Video za Ziada

Viunganishi ya Haraka

  • Facility Financial Accounting and Reporting System(FFARS)
  • Log in PlanRep System
  • PlanRep Documents
  • FFARS USER GUIDE
  • MANYARA REGIONAL WEBSITE
  • UTUMISHI PORTAL

link tunazolandana

  • TOVUTI YA IKULU
  • MFUMO WA VIBALI YA KUSAFIRI NJE (LIVE)
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA TAMISEMI
  • BARAZA LA MTIHANI LA TAIFA TANZANIA
  • TOVUTI YA HABARI MAELEZO

Watembeleaji wa Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Uelekeo wa Ramani

Wasiliana nasi

    Mbulu district Coucil

    Anuani: P.O.BOX 74

    Simu ya mezani: +255743583078

    Simu: +255716992222

    Barua pepe: md@mbuludc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Awali
    • Kanusho
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.