Na. Nashon Biseko, Mbulu Dc
Kikao Maalum kwaajili ya Maandalizi ya Bajeti ya kitengo cha lishe kwa mwaka wa fedha 2026/2027 kimefanyika katika ukumbi Mdogo wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu leo 15/12/2025 kikihudhuliwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ndugu Juma Kilimba, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya Dkt. Shadrack Makonda, Maafisa Lishe na Watalamu mbalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya.
Aidha Vipaumbele vya bajeti hii vimelenga Kuimarisha upatikanaji wa Dawa na bidhaa za Lishe, Kuimarisha siku ya Afya na Lishe ngazi ya Kijiji, Kuimarisha mfumo wa utoaji Madini, Vitamini na Dawa za Minyoo ya Tumbo, Matumizi ya vyakula vilivyorutubishwa Kibailojia, Kuimarisha mfumo wa Elimu ya Lishe katika siku 1,000 za Mtoto, Kuimarisha miradi ya bustani za mbogamboga, miti ya matunda pamoja na mazao yaliyorutubishwa kibaolojia shuleni ( msingi na sekondari) n.k


Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.