MAKADIRIO YA BAJETI YA LISHE KWA MWAKA 2025//26 YAFIKA MIL.68.
Na, Ruth Kyelula, Mbulu DC.
Afisa Lishe wa Wilaya, Jackline David amesema kuwa kwa mwaka ujao wa fedha 2025/26 Kitengo cha Lishe wametengewa milioni 68 na Halmashari kwa ajili ya kutekeleza afua mbali mbali za Lishe kwa kuzingatia vipaumbele mbali mbali vya Halmashauri ikiwemo kupunguza utapia mlo makali na udumavu katika jamii kwa watoto chini ya miaka mitano.
Picha ya pamoja ya wajumbe wa Kikao cha makadirio ya bajeti ya Lishe.
Hayo yalisemwa na Afisa Lishe wa Wilaya, Jackline David, wakati wa kikao cha kupitia makadirio ya bajeti ya mwaka wa fedha 2025/26, yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri, Desemba 10, 2024.
“Kitu kikubwa ambacho tumepanga kufanya kwa mwaka ujao ni elimu kwa sana kwenye jamii ili tuweze kukabiliana na matatizo mbalimbali kwa sababu kuna jamii inafuga, inalima lakini hawana uelewa wa nini kifanyike, mtu unakuta ana chakula lakini unakuta ana mtoto ana utapiamlo, lakini ukimuuliza mnalima nini anajibu kila kitu lakini mtoto anampa ugali na maziwa na kwa hali hiyo lazima mtoto apate utapia mlo.” Alisema Afisa Lishe.
Baadhi ya washiriki wa Kikao cha Lishe
Aidha Afisa lishe wamewaomba idara mtambuka wanazofanya nazo kazi, mfano idara ya Kilimo,mifugo, Maendeleo ya jamii, Ustawi na wengine kwenye shughuli zao wanazofanya, waweke kipengele cha Lishe wanapo enda kwenye jamii na kwenye bajeti zao waweke kipengele cha Lishe ili waweze kuipandisha bajeti ya Lishe ya Halmashauri na ili ionekane inatekeleza afua za Lishe.
Afisa lishe amewaomba wataalamu wafanye kazi kwa kushirikiana,lakini pia huko kwenye jamii wanakoenda kutoa elimu, wazingatie elimu wanayopewa .Kwahiyo maelekezo wanayopewa wayazingatie, wayafanyie kazi,wayatekeleze na waachane na Imani potofu za mtoto akipata utapiamlo wanasema kalogwa.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.