Na, Ruth Kyelula, Mbulu - DC
Mkuu wa wilaya ya Mbulu, Veronica Kessy amewataka Madiwani kusimamia mipango mizuri inayopangwa na Halmashauri pamoja na kuwapongeza kwa kuendelea kuongoza katika ukusanyaji wa mapato ya ndani katika Halmashauri zote za mkoa wa Manyara.
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Veronica Kessy akizungumza na Baraza la Madiwani
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Veronica Kessy, wakati akizungumza na Madiwani pamoja na wataalamu katika kikao cha Baraza la Madiwani kwa robo ya kwanza Julai mpaka septemba, kilichofanyika Oktoba 30, 2024 katika ukumbi wa Halmashauri.
“Katika mapato ya ndani hayo ndio tutapata fedha ya uendeshaji wa Halmashauri, lakini humo humo tutoe asilimia arobaini kwenda kupeleka katika miradi kwa mujibu wa maelekezo na taratibu za serikali, lakini pia kama tumekusanya vizuri tujitahidi kudhibiti matumizi ya fedha hizi.” Alisema Mhe. Kessy.
Kamati ya usalama ya wilaya pamoja na wataalamu wakifuatilia Kikao hicho cha Baraza.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Joseph Mandoo amewaasa waheshimiwa Madiwani, wataalamu, watendaji wa kata na vijiji kuwa na jukumu la kuhakikisha fedha zilizoletwa na Mhe. Rais zinatumika kwa wakati na lazima thamani ya fedha ionekane kulingana na majengo yanayojengwa na ubora wa majengo.
Makatibu wa vikao wakifuatilia Baraza.
Aidha amewaomba waheshimiwa Madiwani na wataalam, wafanye kazi kwa kushirikiana kwa karibu na Mkuu wa Wilaya kwa sababu ana uzoefu mkubwa kwenye serikali za mitaa, kwa hiyo wafahamu hilo ili waweze kufanikisha maendeleo ya Halmashauri.
Waheshimiwa Madiwani wakifuatillia kikao cha Baraza
“Niwaombe waheshimiwa Madiwani tuwe mstari wa mbele, mahali mradi unajengwa tusibanduke pale tuangalie nini kinafanyika, tupitie pia na taarifa za manunuzi, tuone kama vifaa vinavyonunuliwa vinaendana na bei ya soko. Tuhakikishe haya yote yanafanyika ili tuweze kufanikisha shughuli za maendeleo kwenye Wilaya yetu na miradi yetu ikamilike kwa wakati.” Alisema Mandoo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Abubakar Kuuli alisema kuwa kwa upande wa makusanyo ya mapato ya ndani, halmashauri bado inaendelea vizuri.
Mkurugenzi wa Halmashhauri ya Wilaya ya Mbulu akitoa hotuba yake kwenye kikao cha Baraza la Madiwani
“Hata katika hii robo ya kwanza, mpaka tunafika September hadi leo tumefika asilimia takribani 35%, lakini lengo letu lilikuwa kukusanya asilimia 31.8, kwahiyo tumezidi asilimia takribani tatu. Kwahiyo tunaenda vizuri.” Alisema Mkurugenzi Kuuli.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.