Na, Magreth Mbawala, Mbulu DC.
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mhe.Michael Semindu leo Julai 31,2025 amekabidhi vyeti vya pongezi kwa vijana 130 wa hamasa walioshiriki katika mapokezi na kuukimbiza Mwenge wa Uhuru 2025.
Hayo yamefanyika mapema leo katika viwanja vya Haydom huku zoezi hilo likiwa limetanguliwa na Jogging,usafi wa mazingira Kituo cha polisi na stendi ya zamani,kugawa vyeti na mwisho kushiriki chai ya pamoja.
“Nawaahidi nyinyi nyote mtakwenda Mkoani Mbeya mwezi Oktoba kwenda kuzima Mwenge wa Uhuru,hivyo mjiandae vema”.alisema Mhe.Semindu.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndugu Abubakar Kuuli, aliwapongeza sana hamasa kwa ushiriki mzuri kwenye Mwenge wa Uhuru na kuwaambia kuwa wanawahitaji sana kwenye matukio mengi na sio Mwenge tu hivyo waendelee na mazoezi wasikae tu.
Aidha,Mratibu wa Mwenge wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Edes Melly alisema wametoa vyeti hivyo vya pongezi kama motisha kwa vijana na pia kutii agizo la mkimbiza Mwenge kitaifa Ndugu Ismail Ally Ussi kuwa juhudi za vijana wa hamasa zitambulike.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.