Na, Magreth Mbawala, Mbulu DC.
Mbunge wa Viti Maalum kupitia kundi la wafanyakazi, Dr. Alice Karungi Kaijage amewataka wafanyakazi wote waliojiandikisha kwenye daftari la kupiga kura Kwenda kupiga kura ifikapo Novemba 27,2024. Na kuwaasa kuwa uchaguzi utakaofanyika ni muhimu kwao kwa sababu maamuzi mengi yanatokea huko chini na wanaishi nayo.
Mkuu wa Idara ya Utumishi, Neema Aligawesa akitambulisha watumishi kwa mgeni rasmi.
Aliyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Novemba 13, 2024, katika ukumbi wa Halmashauri.
Aidha akiwa kwenye ziara yake ya kikazi alisema amekuja kuwaona na kuwasikiliza wafanyakazi kujua changamoto mbalimbali ili aweze Kwenda kuzisemea bungeni na kwenye mamlaka husika ili ziweze kupata utatuzi.
“Rais wetu Dr samia Suluhu Hassan ni msikivu sana na ndio maana mambo mengi anayatekeleza”. alisema Dr. Alice.
Akaendelea kwa kusema kuwa miaka mitano nyuma watu walikua hawapandi madaraja ya kazi wala ajira mpya hazikuwepo ila Rais wetu mpendwa ametekeleza hayo kwa asilimia kubwa sana.
Mmoja wa viongozi wa Vyama vya wafanyakazi akiuliza swali kwa mgeni rasmi.
Kwa upande mwingine Mhe. Mbunge aliahidi kuzichukua kero mbalimbali ambazo zimejitokeza kwa wafanyakazi ikiwemo suala la kikokotoo, miundo ya nafasi kwenye Halmashauri na bima ya afya NHIF kuzifikisha bungeni na kwenye Wizara husika kwa ajili ya utatuzi.
Picha ya pamoja ya watumishi wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu pamoja na Mbunge Viti maalum Dr. Alice Kaijage.
Naye kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Joseph Sambo, alimshukuru sana Mhe. Mbunge Kaijage kwa kuwatembelea na kushirikishana changamoto mbalimbali za kiutumishi, pia alimkaribisha tena Mbulu DC.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.