Mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Dr. Shadrack Makonda amekabidhi vifaa tiba vya shilingi 1,000,000 kwa fundi sanifu Tarehe 01.10.2025.
Vifaa hivi vimekabidhiwa katika ofisi ya Mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu iliyopo katika jengo la Halmashauri.
“Fedha zilizotumika kununua vifaa hivi ni za uboreshaji idara ya afya kwa hiyo vifaa hivi vitamsaidia fundi sanifu kufanya kazi zake za ufundi wa vifaa tiba kwa ufanisi” Alisema Makonda.
Aidha, Makonda amemtaka fundi sanifu kutatua changamoto za vifaa kwenye Hospitali,vituo vya afya na Zahanati.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.