• Mlalamikaji |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Mbulu District Council
Mbulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Taasisi
    • Orodha ya Wakurugenzi
  • Utawala
    • Idara
      • Idara ya utumishi na mahusiano
      • Mipango, Takwimu na Uangalizi
      • Idara ya Fedha
      • Elimu na Utamaduni
      • Afya
      • Kilimo.Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na uthibiti wa taka ngumu
      • Uvuvi na Ufugaji
      • Idara ya Ujenzi na Zimamotto
        • Moto
      • Idara ya Maji
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Goverment Communication
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Miongozo
    • Sheria
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Picha Jongefu
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
  • Miradi
    • Miradi iliyopitishwa
    • Miradi inayoendela
    • Miradi iliyokamilika
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Dinamu
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Uchumi
      • Kamati ya Ardhi
      • Kamati ya ALAT
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba za Vikao
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Sekta ya Viwanda
    • Sekta ya Kilimo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Elimu

Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere Aupongeza Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kwa Kupata Hati Safi kwa Mwaka wa Fedha wa 2019/2020 Katika Kikao Maalumu cha Kujadili Hoja za Ukaguzi Leo Tarehe 03.06.2021

Kurushwa hewani: June 3rd, 2021

Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere Akizungumza Katika Baraza Maalumu la Madiwani Lililojadili Hoja za Ukaguzi  kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Katika Kikao Kilichofanyika Ukumbi wa Gote, Dongobesh - Mbulu 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga Akitambulisha Makundi Mbalimbali Katika Kikao Hicho.

Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt. Chelestino Simbalimile Mofuga Akitoa Salamu Katika Kikao Hicho.

Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mh.J.G.Mandoo Akifungua Kikao cha Baraza Hilo.

Mlezi wa Mkoa wa Manyara kwa Serikali za Mitaa Toka Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Kibasa Akizungumaza Katika Kikao Hicho.

Mwandishi wa Vikao Vya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Mlokozi Akisoma Hoja Mbalimbali za Ukaguzi Katika Kikao Hicho.

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Bw. Kaganda Akizungumza Katika Kikao Hicho.

Picha za Wah. Madiwani


Picha za Wataalam

Picha ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga na Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere Baada ya Kikao Hicho








~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~   HABARI KAMILI   ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~





Haya yamejiri leo tarehe 03.06.2021 katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani kilichohusu kujadili hoja zilizoibuliwa na Mkaguzi Mkuu wa serikali za mitaa kwa mwaka 2019/2020 kilichofanyika katika kituo cha elimu cha Gote kilichopo Kata ya Dongobesh Wilayani Mbulu.

Mh. Mkuu wa Mkoa M.Nyerere amesema ni heshima kubwa sana kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa nikiwa mtoto wa Rais wa baba wa Taifa Mwalimu J.K.Nyerere na kwamba watu wote wasiwe na wasiwasi mimi ni mwakilishi wa Mh.Rais Samia Suluhu Hassan hivyo niko kwa ajili yenu naomba mnitume.

Aliongeza kwa kusema lazima kuongoza vizuri, tusiwaongoze vibaya kwani kila ngazi ya uongozi itawaharibia walioko chini yao kwani  hiyo kwa wale wa ngazi ya mwisho ujue kabisa watawanyayasa wananchi.

Mh. Rais alikaa na wazee wa Dar es salaam kwa niaba ya wazee wote nchini, akiwaambia mambo kadhaa ya msingi likiwemo kuwabadilisha baadhi ya viongozi katika ngazi mbalimbali kwa nia njema kabisa ya kuboresha utendaji kazi wa kila siku wa serikali hivyo msiwe na hofu kila kitu kinakwenda vizuri.

Kwa mujibu wa sheria namba 19 kifungu cha 5 Mkuu wa Mkoa atasimamia shuguli zote za ndani ya Mkoa husika kwa maendeleo mapana ya watu wake ikiwa ni pamoja na kufuatilia matumizi na mapato ya wilaya zote katika Mkoa ninaousimamia.

Katika taarifa ya Mkaguzi ya hesabu kama ilivyowasilishwa na Mkaguzi wa hesabu za serikali za mitaa kwa mkoa wa manyara ni kutoa maoni huru kwa hesabu za Halmashauri ili kujiridhisha kama fedha zilizokusanywa zilitumika kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu sahihi. Pia kwa upande wa manunuzi ni kujiridhisha kama manunuzi husika yalifuata sheria, kanuni na taratibu za manunuzi.

Katika miradi ya maendeleo ukaguzi unafanyika kuangalia ubora wa miradi husika kama inaendana na thamani halisi ya fedha iliyotumika. Kitu ambacho ni sahihi kabisa kwa hiyo siyo kukosoa tu bali ni kushauri nini cha kuboresha ili kuimarisha mifumo ya makusanyo ya fedha, matumizi, na usimamizi wa miradi hii katika uwekezaji ili wananchi wapunguziwe kero mbalimbali zinazowakabili. Mh. Mkuu wa Mkoa M.Nyerere ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kwa kupata hati safi kwa miaka 3 mfululizo haya ni matokeo mazuri ya utendaji kazi kati ya madiwani na wataalam wa  halmashauri ya wilaya ya Mbullu.

Hata hivyo maeneo yenye mapungufu yafanyiwe kazi na hoja hizi 11 zilizobaki za mwaka wa fedha 2019/2020 ziendelee kufanyiwa kazi ili ziishe. Mh. Mkuu wa Mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere ameahidi anapanga kutembelea kila Wilaya katika Mkoa huu siku 5 kwa kila Wilaya kukagua na kujadiliana kero, changamoto na namna ya kuzitatua.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga ameishukuru sana Serikali ya awamu ya 6 inayoongozwa na Mh.Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendekea kuwajali wananchi wa Halmashauri ya Mbulu kwa kuleta fedha nyingi ambazo hazikuwepo kwenye bajeti kwa baadhi ni milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Kata ya Eshkesh, milioni 220 kwa ajili ya zahanati kisha milioni 210 kwa ajili ya ununuzi wa gari la mkurugenzi.

Viongozi wote Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. HUdson Kamoga, Mbunge wa Jimbo la Mbulu Mh. Flatei, Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mh.J.G.Mandoo na Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt. Chelestino Simbalimile Mofuga wamemueleza Mh. Mkuu wa Mkoa changamoto zilizopo kubwa ni uchache wa watumishi katika idara mbalimbali lakini idara zilizoathilika sana ni Ujenzi kwa kutokuwa na Mkadiriaji wa Majengo "Quantity Surveyor" lakini pia Mhandisi wa Ujenzi kuwepo 1 anachoka sana hivyo kupelekea baadhi ya miradi kuchelewa kuanza kwa sababu hana muda wa kufika eneo husika kutokana na miradi kuwa mingi sana. Idara ya Pili ni ya Fedha na biashara wapo wahasibu wawili tu mpaka sasa hivyo ukusanyaji wa mapato kuwa shida na viti vingine vya kitaalamu kufanywa kwa kutumiamuda mrefu sana kutokana na uchache huu wa watumishi.

Matangazo

  • Tangazo la fursa za mafunzo ya ufundi stadi awamu ya saba February 01, 2025
  • TANGAZO LA ZABUNI YA UCHIMBAJI VISIMA January 29, 2019
  • JINSI YA KUTOA/KUTUMA MALALAMIKO KWA NJIA YA MTANDO HALMSHAURI YA WILAYA YA MBULU. March 23, 2019
  • KARIBU MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU 2021 June 10, 2021
  • Tazama zote

Habari za hivi Punde

  • MBULU DC YATOA SADAKA KITUO CHA AFYA DONGOBESH.

    January 30, 2025
  • MBULU DC YAKWAMUA VIKUNDI VYA VIJANA KIUCHUMI

    February 13, 2025
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA BAJETI YA BILIONI 38.7 KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026

    February 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI LAHIMIZA WANAFUNZI WARIPOTI SHULENI

    January 31, 2025
  • Tazama zote

Picha Jongefu

MBULU DC KUKUSANYA ZAIDI YA MIL.90 KATIKA MSIMU MPYA WA UVUVI KUTOKA BWAWA LA BONDELA YAEDA CHINI
Video za Ziada

Viunganishi ya Haraka

  • Facility Financial Accounting and Reporting System(FFARS)
  • Log in PlanRep System
  • PlanRep Documents
  • FFARS USER GUIDE
  • MANYARA REGIONAL WEBSITE
  • UTUMISHI PORTAL

link tunazolandana

  • TOVUTI YA IKULU
  • MFUMO WA VIBALI YA KUSAFIRI NJE (LIVE)
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA TAMISEMI
  • BARAZA LA MTIHANI LA TAIFA TANZANIA
  • TOVUTI YA HABARI MAELEZO

Watembeleaji wa Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Uelekeo wa Ramani

Wasiliana nasi

    Mbulu district Coucil

    Anuani: P.O.BOX 74

    Simu ya mezani: +255743583078

    Simu: +255716992222

    Barua pepe: md@mbuludc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Awali
    • Kanusho
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.