• Mlalamikaji |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Mbulu District Council
Mbulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Taasisi
    • Orodha ya Wakurugenzi
  • Utawala
    • Idara
      • Idara ya utumishi na mahusiano
      • Mipango, Takwimu na Uangalizi
      • Idara ya Fedha
      • Elimu na Utamaduni
      • Afya
      • Kilimo.Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na uthibiti wa taka ngumu
      • Uvuvi na Ufugaji
      • Idara ya Ujenzi na Zimamotto
        • Moto
      • Idara ya Maji
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Goverment Communication
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Miongozo
    • Sheria
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Picha Jongefu
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
  • Miradi
    • Miradi iliyopitishwa
    • Miradi inayoendela
    • Miradi iliyokamilika
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Dinamu
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Uchumi
      • Kamati ya Ardhi
      • Kamati ya ALAT
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba za Vikao
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Sekta ya Viwanda
    • Sekta ya Kilimo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Elimu

Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Sezaria V. Makota Atimiza Azma ya Viongozi Wote Kuchanjwa Ili Kuwa Mabalozi Wazuri Katika Uhamasishaji wa Chanjo ya UVIKO 19 Kwa Jamii.

Kurushwa hewani: September 27th, 2021

Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Sezaria V. Makota Akifungua Kikao cha Kamati ya Wilaya cha Uhamasishaji wa Chanjo ya UVIKO 19.



Kama Unavyoona ni Mwendo wa Kuchanja tu Viongozi Wote wa Wilaya ya Mbulu.

Wakufunzi wa Mafunzo Hayo.

Viongozi wa Dini Wakichangia Mada Zilizowasilishwa.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. M.Faraay.


Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Sezaria V. Makota Akisikiliza Mafundisho Haya ya Uhamasishaji.

Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Sezaria V. Makota Akifunga Kikao cha Kamati ya Wilaya cha Uhamasishaji wa Chanjo ya UVIKO 19.








~~~~~~~~~~~~~~~~~~~     HABARI KAMILI    ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~ 




Haya yamejiri leo katika kikao cha Kamati ya UVIKO 19 ya Wilaya ya Mbulu Vijijini kilichofanyika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbulu ambaye Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Sezaria V. Makota Alikuwa ndiyo mwenyekiti wa Kikao na kamati hiyo.


Katika Kikao hicho wakufunzi ni wataalamau wa afya toka OR - TAMISEMIM, mkoani Manyara na Halmashauri ambao wamebobea katika masuala ya utabibu na mafunzo ya chanjo pia. Wahusika katika kikao hiki ni Wataalamu wa afya, baadhi ya wakuu wa Idara na vitengo, wazee maarufu, mwakilishi wa wafanya biashara, viongozi wa dini mbalimbali, kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya.


Hii imepelekea wahusika walioshiriki kikao hicho kupata  elimu ya UVIKO 19 kwa kina na pina.kimsingi hadi kufikia jaana tarehe 26.09.2021 Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Vijijini imechanja watu wapata 514 huku zoezi la uhamasishaji kimkakati linaendelea kwa kasi kuanzia kwenye mikutano ya vijiji na vitongoji ya hadhara, minada na baadaye nyumba kwa nyumba, huku vituo vyote 26 vya kutolea huduma ya afya vinatoa pia chanjo ya UVIKO 19 bure kabisa.


Katika kuhakikisha watu wote wanaelewa kwa undani ni kwamba chanjo hii ni salama, na serikali inawajali wananchi wake ndiyo maana inafanya hii chanjo kuwa ya muhimu kwa maslahi mapana ya nchi yetu. Chanjo hii ilitathminiwa na chuo Kikuu cha kilimo cha Sokoine (SUA) kwa kutumia wataalamu waliotopea na kubobea katika chanjo huku wakitumia vifaa vya kimamboleo vyenye teknolijia ya kisasa vya kuchanganua kwa undani chanzo husika.


Aina ya chanjo zilizoidhinishwa baada ya uchambuzi huu ni Pfizer-BioNTech, Moderna, Oxford-AstraZeneca, Sinopharm na Johnson & Johnson ambapo kwa sasa chanjo iliyopo ni Johnson & Johnson ndiyo inayochanjwa kwa sasa hapa Tanzania na hizo zingine zitafika kwa hapo baadaye.


Kuna mambo 3 ya msingi nayo ni kwanza utafiti ulianza tangu miaka ya mwanzoni mwa 2000 ambapo kulitokea na ugonjwa wa virusi kama huo yaani SARS, MERS na mengine mengi kiasi kwamba aina ya kirusi huyu wataalam walifanya utafiti wa kutosha kwa wakati huo ila  waliacha kuendelea na utafiti baada ya ugonjwwa husika kupotea katika nzchi za urabuni. Lapili ni kutumika kwa vifaa na teknolojia ya kisasa ambapo kwa zamani ingechukua muda mrefu sana kuchambua nini hasa mdudu tabia za mdudu husika na tumthibiti vipi. Cha tatu ni ugonjwa kuenea kwa kasi kwa binadamu hivyo kupelekea hata utafiti wa ugojwa huu kwenda haraka kwasababu ya kupata majibu kwa watu wengi zaidi wanaougua kwa muda mfupi, Cha nne ni kuona watu wanafariki sana hivyo kupelekea kuwepo kwa hii chanzo ili kunususru maisha ya wananchi duniani.


chanjo hii ni salama kwa rika na jinsi tofauti kama vile wazee, kina mama, vijana, wenye magojwa sugu na haina madhara hata kwa mwanamke mwenye mimba na anayenyonyesha ndiyo hasa inamkinga na mtoto pia.

watu wanapaswa kuchanjwa kwasababu ya kuongeza kinga, na kutokuwa mbebaji wa virusi kupeleka kwenye familia, wagonjwa wengine hospitalini, wanafunzi, abiria wanaosafiri kwenye vyombo mbalimbali, kulinda watalii na hatimaye kuuwezesha uchumi wa nchi yetu kutoporomoka zaidi, kwani hakuna mtalii kutoka nje atapenda atumie usafiri ambao anajua wahusika hawajachanjwa.


Hata hivyo Mh. Mkuu wa Wilaya huyo, ameishukuru serikali kwa kuwajali wananchi wa Wilaya ya Mbulu hadi kuwaletea chanjo hii kwa maslahi mapana ya familia zao na taifa kwa ujumla, hivyo kama Wilaya tuko kimkakati zaidi tunahamasisha kwa kila mtu  kuchanjwa ili tuvuke lengo la 60%. Na amewaasa wataalamu wa afya na kamati ya UVIKO 19 kwa ujumla wao kwamba ni lazima uchanjwe wewe muhusika ili uwe balozi mzuri wa kuwahamasisha wananchi kupata chanjo.





Matangazo

  • Tangazo la fursa za mafunzo ya ufundi stadi awamu ya saba February 01, 2025
  • TANGAZO LA ZABUNI YA UCHIMBAJI VISIMA January 29, 2019
  • JINSI YA KUTOA/KUTUMA MALALAMIKO KWA NJIA YA MTANDO HALMSHAURI YA WILAYA YA MBULU. March 23, 2019
  • KARIBU MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU 2021 June 10, 2021
  • Tazama zote

Habari za hivi Punde

  • MBULU DC YATOA SADAKA KITUO CHA AFYA DONGOBESH.

    January 30, 2025
  • MBULU DC YAKWAMUA VIKUNDI VYA VIJANA KIUCHUMI

    February 13, 2025
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA BAJETI YA BILIONI 38.7 KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026

    February 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI LAHIMIZA WANAFUNZI WARIPOTI SHULENI

    January 31, 2025
  • Tazama zote

Picha Jongefu

MBULU DC KUKUSANYA ZAIDI YA MIL.90 KATIKA MSIMU MPYA WA UVUVI KUTOKA BWAWA LA BONDELA YAEDA CHINI
Video za Ziada

Viunganishi ya Haraka

  • Facility Financial Accounting and Reporting System(FFARS)
  • Log in PlanRep System
  • PlanRep Documents
  • FFARS USER GUIDE
  • MANYARA REGIONAL WEBSITE
  • UTUMISHI PORTAL

link tunazolandana

  • TOVUTI YA IKULU
  • MFUMO WA VIBALI YA KUSAFIRI NJE (LIVE)
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA TAMISEMI
  • BARAZA LA MTIHANI LA TAIFA TANZANIA
  • TOVUTI YA HABARI MAELEZO

Watembeleaji wa Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Uelekeo wa Ramani

Wasiliana nasi

    Mbulu district Coucil

    Anuani: P.O.BOX 74

    Simu ya mezani: +255743583078

    Simu: +255716992222

    Barua pepe: md@mbuludc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Awali
    • Kanusho
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.