• Mlalamikaji |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Mbulu District Council
Mbulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Taasisi
    • Orodha ya Wakurugenzi
  • Utawala
    • Idara
      • Idara ya utumishi na mahusiano
      • Mipango, Takwimu na Uangalizi
      • Idara ya Fedha
      • Elimu na Utamaduni
      • Afya
      • Kilimo.Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na uthibiti wa taka ngumu
      • Uvuvi na Ufugaji
      • Idara ya Ujenzi na Zimamotto
        • Moto
      • Idara ya Maji
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Goverment Communication
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Miongozo
    • Sheria
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Picha Jongefu
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
  • Miradi
    • Miradi iliyopitishwa
    • Miradi inayoendela
    • Miradi iliyokamilika
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Dinamu
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Uchumi
      • Kamati ya Ardhi
      • Kamati ya ALAT
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba za Vikao
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Sekta ya Viwanda
    • Sekta ya Kilimo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Elimu

Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt. Chelestino Simbalimile Mofuga Awaasa Wananchi wa Haydom Katika Mkutano wa Hadhara Uliofanyika Viwanja vya Kata ya Haydom Kufanya Kazi za Maendeleo Muda wa Siasa Umekwisha Leo Tarehe 12.03.2021

Kurushwa hewani: March 12th, 2021

Aliyeshika "MIC" ni Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt.Chelestino Simbalimile Mofuga Akifungua Mkutano wa Hadhara wa Wananchi  wa Haydom

Aliyeshika "MIC" ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu 

Ndugu Hudson S. Kamoga Akisalimia Wananchi na Kumkaribisha Mh. Mkuu wa Wilaya ya Mbulu.

Aliyeshika "MIC" ni Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt. C.S. Mofuga Kitoa Ufafanuzi wa Kero Mbalimbali Zilizotolewa na Wananchi wa Kata ya Haydom



Aliyeshika "MIC" ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndugu Hudson S. Kamoga kwa Nyakati Tofauti Akitoa Ufafanuzi wa Masuala Mbalimbali Yaliyojitokeza Katika Mkutano Huo.


Picha za Hapo Juu ni za Wataalamu Mbalimbali Wakuu wa Idara na Vitengo Pamoja na Watumishi Wengine wa Kiserikali wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Katika Mkutano Huo.





Picha za Hapo Juu ni Baadhi ya Wananchi Waliouliza na Kutoa Maoni Mbalimbali Mbele ya  Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt.Chelestino Simbalimile Mofuga Katika Mkutano Huo.


Aliyeshika "MIC" ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Haydom Ndugu Elihuruma Akijibu Maswali Yaliyoulizwa na Wananchi Katika Mkutano Huo.

Aliyeshika "MIC" ni Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili Akitoa Ufafanua wa Masuala ya Ardhi Yaliyojitokeza  Katika Mkutano Huo.


Aliyeshika "MIC" ni Mwakilishi wa Meneja wa Wakala wa Maji Mjini na Vijijini "RUWASA" Ndugu John Ombay Akitoa Ufafanua wa Masuala ya Maji Yaliyojitokeza  Katika Mkutano Huo.

Aliyeshika "MIC" ni Meneja wa Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini "TARURA" Nuru Hondo Akitoa Ufafanua wa Masuala ya Barabara Yaliyojitokeza  Katika Mkutano Huo.



Picha za Hapo Juu ni za Wananchi Waliohudhuria Katika Mkutano Huo






~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~    HABARI KAMILI    ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~    


Hayo yamejiri leo katika mkutano mkuu wa hadhara wa wananchi wa kata ya Haydom ambapo mgeni rasmi alikua ni Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt. Mofuga. Dhumuni kubwa mkutano huu ni kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua ikiwa ni agizo la Mh.Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joseph Mkirikiti baada ya kupata taarifa kuwa hawakuridhika na majibu ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndugu H.S.Kamoga pamoja na wakuu wa idara na vitengo katikamkutano mkuu wa hadhara wa tarehe 03.03.2021 uliosikiliza  kero za wananchi na kuzitolea ufumbuzi wa uhakika.

Kimsingi mkutano wa leo ulikuwa wa manufaa chanya kwa wananchi wa haydom kwani kero mbalimbali za kisekta zilisikilizwa na kutolewa maamuzi hapo hapo zikiwemo za maji, barabara, elimu, ardhi na afya. Hata hivyo, wananchi wa Haydom katika mkutano huo wa hadhara mbele ya Mh. Mkuu wa Wilaya walimpongeza sana Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndugu Hudson S. Kamoga kwa kuwa msikivu, mnyenyekevu na mwenye huruma kwa kila mwanachi kwa kusikiliza kero na kuzitolea ufafanuzi wa uhakika na ulioridhisha hivyo wapuuze kikundi cha watu wachache chenye nia mbaya ya kuvuruga maendeleo ya Haydom wakati wao si wakazi wa hapa Haydom.  


Awali Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt. Chelestino Simbalimile Mofuga alitangulia kwa kuwauliuliza wananchi wa Haydom katika mkutano huo kama waliteua kikundi maalumu cha kwenda ngazi ya mkoa kuwasilisha kero zao badala ya kwenda ngazi ya Mkuu wa Wilaya baada ya wachache hao kudai kutoridhika na majibu ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu katika mkutano mkuu wa tarehe 03.03.2021 uliofanyika viwanja vya Ofisi ya Kata ya Haydom. Wananchi kwa kauli moja walijibu hatukuwatuma wala serikali ya kijiji hivyo wao ndio walioruka ngazi ya kwenda mkoani.


Hata hivyo, mgeni rasmi huyo alimpongeza sana Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ndugu Hudson S. Kamoga kwa kuwajali wananchi kwa kuja kuwasikiliza, kutoa ufafanuzi, miongozo  na kutoa maamuzi juu ya kero zilizowasilishwa kwakekupitia mkutano huo.

Katika mjadala uliochukua takribani masaa zaidi ya 7 Mh.Mkuu wa Wilaya huyo alifikia maazimio haya ili kukamilisha utekelezwaji wa kero hizi.

Kwa vijiji vyote kila kijiji kuwe na na daftari la makazi ili kuwasajiri watu wote wanaoingia na kuishi Wilaya ya Mbulu ,pia mhusika ajulikane na serikali ya kijiji na mkutano mkuu kuwa katoka wapi na anafanya nini na kila gesti kwa kila mtu anayelala sharti arekodiwe kwenye daftari la wageni kwa usalama wa Wilaya yetu. Tunakaribisha watu mbalimbali kufanya biashara hapa lakini kwa kufuata taratibu za nchi yetu ili biashara ziendelee kufanyiaka bila wasiwasi.

Alimuagiza meneja wa Wakala wa Maji Mjini na Vijijini "RUWASA" kufanya hesabu za kitaalamu juu ya miradi ya maji ya Mbulu Mji na Haydom kisha kuileta katika kamati ya ulinzi na usalama.

Kuhusiana na maji, Meneja wa RUWASA ahakikishe kifaa cha kusukuma maji "motor" ikiharibika basi isizidi siku 5 iwe imerekebishwa na pia kama ni manunuzi yawe yameshafanyika kwani kukosa maji kutapelekea mlipuko wa magonjwa lakini pia hapa pana biashara pia zinazohitaji maji muda wote.

Meneja wa Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini "TARURA" bwana Nuru Hondo alitamka kuwa wameshapokea karibu bilioni 1.2 mwaka huu ikiwa ni fedha za kujenga barabara za lami, za vumbi na mifereji yake kwa hiyo Haydom itapendeza.

Mkaguzi wa ndani ahakikishe anafanya ukaguzi wa kutosha katika kamati za wananchi za kupokea na kugawa chakula mashuleni kwa Wilaya nzima kisha kushauri njia itakayowawezesha kujiendesha kwa ufanisi na kupunguza migogoro isiyo ya lazima inayotookana na matumizi ya chakula husika.









Matangazo

  • Tangazo la fursa za mafunzo ya ufundi stadi awamu ya saba February 01, 2025
  • TANGAZO LA ZABUNI YA UCHIMBAJI VISIMA January 29, 2019
  • JINSI YA KUTOA/KUTUMA MALALAMIKO KWA NJIA YA MTANDO HALMSHAURI YA WILAYA YA MBULU. March 23, 2019
  • KARIBU MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU 2021 June 10, 2021
  • Tazama zote

Habari za hivi Punde

  • MBULU DC YATOA SADAKA KITUO CHA AFYA DONGOBESH.

    January 30, 2025
  • MBULU DC YAKWAMUA VIKUNDI VYA VIJANA KIUCHUMI

    February 13, 2025
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA BAJETI YA BILIONI 38.7 KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026

    February 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI LAHIMIZA WANAFUNZI WARIPOTI SHULENI

    January 31, 2025
  • Tazama zote

Picha Jongefu

MBULU DC KUKUSANYA ZAIDI YA MIL.90 KATIKA MSIMU MPYA WA UVUVI KUTOKA BWAWA LA BONDELA YAEDA CHINI
Video za Ziada

Viunganishi ya Haraka

  • Facility Financial Accounting and Reporting System(FFARS)
  • Log in PlanRep System
  • PlanRep Documents
  • FFARS USER GUIDE
  • MANYARA REGIONAL WEBSITE
  • UTUMISHI PORTAL

link tunazolandana

  • TOVUTI YA IKULU
  • MFUMO WA VIBALI YA KUSAFIRI NJE (LIVE)
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA TAMISEMI
  • BARAZA LA MTIHANI LA TAIFA TANZANIA
  • TOVUTI YA HABARI MAELEZO

Watembeleaji wa Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Uelekeo wa Ramani

Wasiliana nasi

    Mbulu district Coucil

    Anuani: P.O.BOX 74

    Simu ya mezani: +255743583078

    Simu: +255716992222

    Barua pepe: md@mbuludc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Awali
    • Kanusho
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.