Na, Magreth Mbawala,Mbulu DC.
Wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu wamefanya ziara ya kukagua miradi ya shilingi Bilioni 4,764,666,012 kwa kipindi cha robo ya nne.
Ziara hiyo ilifanyika Tarehe 22-23/09/2025 katika kata mbalimbali ambapo jumla ya miradi thelathini na tatu (33) ilikaguliwa.
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na Ujenzi wa Uzio na ununuzi wa samani kwenye jengo la Halmashauri Mil. 778,ukarabati na ujenzi wa madarasa ya elimu maalum na matundu ya vyoo Shule ya Msingi Dongobesh chini Mil. 163.6, ukamilishaji wa vyumba vya madarasa Shule ya Msingi Laghangesh Mil. 15,ujenzi wa madarasa na matundu ya vyoo Shule ya Msingi Mangisa Mil. 88.6,ukamilishaji wa jengo la utawala na nyumba ya mwalimu shule ya Sekondari Bashay Mil. 40,Ujenzi wa Shule mpya ya amali ya Mkoa Bil. 1.6,ukamilishaji wa vyumba vya madarasa shule ya msingi shikizi Masqaroda Mil. 20,ukamilishaji wa ofisi ya kata ya Masqaroda Mil. 10,ukamilishaji wa vyumba vya madarasa shule ya msingi shikizi Miqaw Mil. 12.5,ujenzi wa nyumba ya Mwalimu shule ya msingi Masieda Mil. 51 na ujenzi wa kituo cha afya kata ya Masieda Mil. 586.
Pia miradi ya ujenzi wa shule mpya ya awali na msingi Dinamu Mil. 330.7,ukamilishaji wa madarasa katika shule ya msingi Genda Mil. 25,ujenzi wa choo cha Zahanati Muslur Mil. 29.4,ukamilishaji wa darasa moja shule ya Msingi Muslur Mil. 15,ukamilishaji wa ofisi ya kata Dinamu Mil. 10,ukamilishaji wa vyumba vya madarasa shule ya Msingi Shikizi Genda Mil. 15,ukamilishaji wa nyumba ya mwalimu na vyumba viwili vya madarasa shule ya Msingi Getagujo Mil. 32.4,ujenzi wa choo na ukamilishaji wa nyumba ya mtumishi kwenye Zahanati Gidmadoy Mil. 29.5,ukamilishaji wa Hostel Shule ya Sekondari Maghang Mil. 50 na ujenzi wa madarasa ya awali,elimu msingi na matundu 12 ya vyoo Mil. 132.8 vilikaguliwa.
Aidha,chanzo cha fedha kwa miradi yote hiyo ni Serikali kuu ,Mapato ya ndani,Boost,SWASH,Sequip,WASH,GPE-Lannes,KOICA na TMCHIP.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.