Na, Magreth Mbawala,Mbulu DC.
Timu ya wataalamu kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara imefanya ziara ya kukagua miradi yenye thamani ya shilingi bilioni 5,330,975,932.80 kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu.
Ziara hiyo imefanyika tarehe 29-30/09/2025 ambapo jumla ya miradi thelathini na sita (36) ilikaguliwa.
Miradi iliyokaguliwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa 3 na matundu 6 ya vyoo Shule ya Msingi Mangisa Mil. 88.6, ukamilishaji wa vyumba 2 vya madarasa Shule ya Msingi shikizi Qatamarish Mil. 20, ukamilishaji wa vyumba 2 vya madarasa Shule ya Msingi Miqaw Mil. 12.5, ujenzi wa kituo cha Afya Masieda Mil. 586, ujenzi wa nyumba ya mwalimu na ukamilishaji wa chumba cha darasa Shule ya Msingi Masieda Mil. 63, ujenzi wa choo cha Wanafunzi Shule ya Msingi Gidhim Mil. 49.4, ukamilishaji wa OPD kituo cha Afya Maretadu Mil. 30, ukamilishaji wa chumba cha maabara Shule ya Sekondari Jakaya Kikwete Mil. 30, ujenzi wa choo cha Wanafunzi Shule ya Msingi Mareba Mil. 38.9,ukamilishaji wa chumba cha maabara Shule ya Sekondari Haydarer Mil. 20 na ukamilishaji wa chumba cha darasa na ujenzi wa vyoo vya Wanafunzi Shule ya Sekondari Geterer Mil. 32.5.
Ujenzi wa Shule mpya ya awali na Msingi katika eneo la Sekondari Dinamu Mil. 330.7, ukamilishaji wa vyumba 2 vya Madarasa Shule ya Msingi shikizi Genda Mil. 15, ukamilishaji wa vyumba 2 vya madarasa Shule mpya ya Msingi Ginyabudel Mil. 25, ukamilishaji wa ofisi ya kata Dinamu Mil. 10, ujenzi wa choo cha Zahanati Muslur Mil 29.4, ujenzi wa choo cha Zahanati Gidmadoy Mil. 27.1, ujenzi wa mabweni 2,madarasa 5 na vyoo matundu 8 katika Shule ya Sekondari Tumati Mil. 401.8, ujenzi wa Shule ya Amali ya Mkoa Bashay Bil. 1.6, ujenzi wa shule ya mkondo mmoja Dumanang Mil. 351, ujenzi wa uzio,ununuzi wa samani na kuweka pavement katika jingo la Halmashauri Mil. 778.2 na ukamilishaji wa nyumba ya Mkurugenzi pamoja na nyumba mbili za wakuu wa idara Mil. 30.
Chanzo cha fedha kwa miradi yote hiyo ikiwa ni mapato ya ndani Mil.216.5, Serikali kuu Bilioni 1.1 na wafadhili na fedha nyingine ikiwemo michango ya wananchi Bilioni 3.9.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.