• Mlalamikaji |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Mbulu District Council
Mbulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Taasisi
    • Orodha ya Wakurugenzi
  • Utawala
    • Idara
      • Idara ya utumishi na mahusiano
      • Mipango, Takwimu na Uangalizi
      • Idara ya Fedha
      • Elimu na Utamaduni
      • Afya
      • Kilimo.Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na uthibiti wa taka ngumu
      • Uvuvi na Ufugaji
      • Idara ya Ujenzi na Zimamotto
        • Moto
      • Idara ya Maji
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Goverment Communication
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Miongozo
    • Sheria
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Picha Jongefu
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
  • Miradi
    • Miradi iliyopitishwa
    • Miradi inayoendela
    • Miradi iliyokamilika
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Dinamu
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Uchumi
      • Kamati ya Ardhi
      • Kamati ya ALAT
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba za Vikao
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Sekta ya Viwanda
    • Sekta ya Kilimo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Elimu

MKUU WA MKOA WA MANYARA Bi. QUEEN SENDIGA AWEKA JIWE LA MSINGI SHULE YA MSINGI FLATEI MASSAY NA KUHANI MSIBA MWALIMU.

Kurushwa hewani: August 18th, 2023


Mkuu wa Mkoa wa Manyara,Bi. Queen Sendiga ameweka jiwe la msingi katika Shule ya Msingi Flatei Massay iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, kata ya Haydom.

Mkuu wa mkoa ameweka jiwe hilo la msingi katika shule ya Flatei Massay mnamo Agosti 17,2023, katika Halmashauri ya wilaya ya Mbulu kata ya Haydom.

Mheshimiwa Queen amewashukuru na kuwapongeza wananchi wa Haydom kwa ushirikiano na Serikali iliyopo madarakani kwa kuunga mkono juhudi za Serikali zilizowekwa katika kata hiyo ambapo wananchi wamechangia zaidi ya shilingi Milioni kumi na Saba katika ujenzi wa shule ya msingi hiyo. Ambapo Serikali imeweka zaidi ya milioni mia tatu arobaini, ambayo itafanya jumla ya gharama ya ujenzi huo kufika milioni mia tatu sitini na sita.

"Kwa mwaka huu wa fedha, kwenye eneo la Elimu Serikali imetutengea zaidi ya bilioni 5.3 kwa ajili ya muendelezo wa miundombinu kwenye sekta ya Elimu , hii ni ujenzi wa shule Mpya hizi mnazoziona lakini ukarabati wa shule ambazo zimeonekana ni chakavu, nyongeza ya matundu ya vyoo, lakini maboresho ya miundombinu mbalimbali kwenye sekta ya Elimu.Tuendelee kumshukuru Mheshimiwa Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoipeleka nchi kwenye muelekeo ule ule ambao Watanzania wote wanatamani kukuona." Alisema Mheshimiwa Queen Sendiga.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Komredi Kheri James amesema kuwa baada ya Mheshimiwa Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kusikia kilio Cha wananchi wa Mbulu juu ya changamoto ya mrundikano wa wanafunzi katika shule ya msingi ya Haydom, ilimpendeza na aliona ni vyema alete fedha ili tupate shule mpya yenye Kila kitu.

Naye Mkuu wa shule ya msingi Haydom Ndugu Joshua Mwambo John amesema kuwa shule ilipokea fedha kiasi Cha shilingi milioni mia 348 na laki tano kutoka Serikali kuu kupitia mradi wa BOOST.Ambapo fedha hizo ziliingizwa kwenye akaunti ya shule tarehe 24/04/2023 na utekelezaji wa mradi ulianza rasmi Mei 30, 2023.

 


" Fedha tulizopokea ni kwa ajili ya ujenzi wa shule yenye mkondo mmoja ikiwa na maana ya madarasa mawili ya mfano, vyoo matundu 16, jengo la utawala pamoja na kichomea taka. Lengo la mradi huu Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa ni kupunguza mlundikano wa wanafunzi darasani katika shule ya msingi ya Haydom ambayo Ina wanafunzi 1882." Alisema Mwalimu Mwambo


Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndugu Joseph Mandoo alisema kuwa wananchi wa Mbulu wanayo faraja kubwa sana wanafunzi waliyokuwa wanalundikana zaidi ya elfu moja mia nane, sasa kwa bahati njema chini ya jemedari Flatei Massay kupeleka kilio cha wana Mbulu kwenda kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan kuomba fedha milioni mia tatu arobaini na nane kujenga shule Mpya ya Haydom ambayo ipo mbioni kukamilika, tunaishukuru sana Serikali.


Aidha Mkuu wa Mkoa, Mheshimiwa Queen Sendiga baada ya kuweka jiwe la Msingi pamoja na msafara wake wote waliungana na mamia ya wakazi wa Haydom kwenda kuhani na kutoa salaam za rambirambi kwa niaba ya Serikali kufuatia  msiba wa mtumishi wa mwenzetu Mwalimu Benedicto S. Nada wa Shule ya Msingi Endaharghadakt kilichotokea mwanzoni wa wiki hii. Kwa pamoja tutaendelea kuyaenzi mazuri yote aliyoyafanya Mwalimu wetu enzi  za Uhai, Roho ya Marehemu ipumzike kwa amani. alisema Bi. Queen.



#KWA PAMOJA TUNAIJENGA MBULU YETU#

Matangazo

  • Tangazo la fursa za mafunzo ya ufundi stadi awamu ya saba February 01, 2025
  • TANGAZO LA ZABUNI YA UCHIMBAJI VISIMA January 29, 2019
  • JINSI YA KUTOA/KUTUMA MALALAMIKO KWA NJIA YA MTANDO HALMSHAURI YA WILAYA YA MBULU. March 23, 2019
  • KARIBU MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU 2021 June 10, 2021
  • Tazama zote

Habari za hivi Punde

  • MBULU DC YATOA SADAKA KITUO CHA AFYA DONGOBESH.

    January 30, 2025
  • MBULU DC YAKWAMUA VIKUNDI VYA VIJANA KIUCHUMI

    February 13, 2025
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA BAJETI YA BILIONI 38.7 KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026

    February 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI LAHIMIZA WANAFUNZI WARIPOTI SHULENI

    January 31, 2025
  • Tazama zote

Picha Jongefu

MBULU DC KUKUSANYA ZAIDI YA MIL.90 KATIKA MSIMU MPYA WA UVUVI KUTOKA BWAWA LA BONDELA YAEDA CHINI
Video za Ziada

Viunganishi ya Haraka

  • Facility Financial Accounting and Reporting System(FFARS)
  • Log in PlanRep System
  • PlanRep Documents
  • FFARS USER GUIDE
  • MANYARA REGIONAL WEBSITE
  • UTUMISHI PORTAL

link tunazolandana

  • TOVUTI YA IKULU
  • MFUMO WA VIBALI YA KUSAFIRI NJE (LIVE)
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA TAMISEMI
  • BARAZA LA MTIHANI LA TAIFA TANZANIA
  • TOVUTI YA HABARI MAELEZO

Watembeleaji wa Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Uelekeo wa Ramani

Wasiliana nasi

    Mbulu district Coucil

    Anuani: P.O.BOX 74

    Simu ya mezani: +255743583078

    Simu: +255716992222

    Barua pepe: md@mbuludc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Awali
    • Kanusho
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.