• Mlalamikaji |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Mbulu District Council
Mbulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Taasisi
    • Orodha ya Wakurugenzi
  • Utawala
    • Idara
      • Idara ya utumishi na mahusiano
      • Mipango, Takwimu na Uangalizi
      • Idara ya Fedha
      • Elimu na Utamaduni
      • Afya
      • Kilimo.Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na uthibiti wa taka ngumu
      • Uvuvi na Ufugaji
      • Idara ya Ujenzi na Zimamotto
        • Moto
      • Idara ya Maji
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Goverment Communication
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Miongozo
    • Sheria
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Picha Jongefu
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
  • Miradi
    • Miradi iliyopitishwa
    • Miradi inayoendela
    • Miradi iliyokamilika
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Dinamu
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Uchumi
      • Kamati ya Ardhi
      • Kamati ya ALAT
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba za Vikao
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Sekta ya Viwanda
    • Sekta ya Kilimo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Elimu

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Katika Kikao cha Baraza la Madiwani Ahimiza Ushirikiano Kati ya Wakuu wa Idara na Madiwani Ili Kuwahudumia Wananchi Tarehe 28.04.2021

Kurushwa hewani: April 28th, 2021

Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mh. Joseph Mandoo Akizungumza Katika Kikao cha Baraza Hilo la Madiwani


Kushoto ni Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt.Chelestino Simbalimile Mofuga Akisamilia Wajumbe wa Baraza la Madiwani

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Ndugu Hudson S. Kamoga Akizungumza Katika Kikao  Hicho


 Mh. Mbunge Flatei wa Jimbo la Mbulu,  Akisalimia na Kuzungumza na Wajumbe wa Baraza la Madiwani

Wah. Madiwani Katika Muonekano wa Picha Tofauti Tofauti Wakiwa kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani


Wakuu wa Idara na Vitengo Katika Muonekano wa Picha Tofauti Tofauti Wakiwa kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani






~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~  HABARI KAMILI   ~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~ 



Haya yamejiri katika  kikao cha baraza la waheshimiwa madiwani cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2020/2021 kuanzia januari, 2021 hadi machi 2021 kilichofanyika katika  ukumbi wa shule ya sekondari ya Gote iliyopo kata ya Dongobeshi, ambapo kubwa ni kuwepo kwa mshikamano wa dhati baina ya wakuu wa idara/vitengo na madiwani kwani bila wataalamu hakuna kitu kitafanyika na bila madiwani hakuna kitu kitapita.


Zaidi imefahamika kwamba ukusanyaji wa mapato hadi machi 2021 ilikua ni kiasi cha milioni mia 9.3 ambayo ni takribani zaidi ya 60% ya makusanyo yote ya mapato kwa mwaka kwa halmashauri ya Wilaya ya Mbulu vijijini, hata hivyo kuongeza kasi zaidi kwa miezi miwili iliyobaki kwa kusimamia mianya ya utoroshaji wa mapato ili kuweza kufikia lengo zuri na kujipanga kwa mwaka wa fedha ujao wa 2021/2022, kwani usimamizi mzuri wa ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri  utasaidia fedha hizi kukuza wigo wa kuwahudumia wananchi wa halmashauri ya wilaya ya mbulu vijijini.


Kwa sasa changamoto zinazojitokeza ni pamoja na barabara kutokuwa rafiki katika maeneo mengi kiasi kwamba uchukuaji wa mazao katika maeneo ya vijijini ili kwenda kuuzwa mjini umekuwa wa shida na hii imepelekea kuongezeka kwa gharama za usafirishaji na kupunguza faida anayopata mkulima kutokana na kuongezeka kwa gharama za usafirishaji mazao husika.


Maeneo kadhaa yaliyosisitizwa kuwa 10% ya makundi maalumu yaani vijana, walemavu na wanawake wapewe kipaumbele katika kuwakopesha mikopo yao ili wajikwamue kiuchumi chamsingi ni kuwafuatilia katika marejesho ya mikopo hiyo.


Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt.Chelestino Simbalimile Mofuga katika kuwasalimia wajumbe alisema "ili kuweza kupunguza na kutokomeza mabango ya wananchi pindi viongozi wa juu wanapokuja yasijitokeze ni kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi kwa kutatua kero zao kwa usahihi na kwa wakati kwa nguvu zote katika maeneo yote kuanzia ngazi ya Kata.


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ndugu Hudson S. Kamoga ameelezea kwamba ukamilishaji wa bweni la shule ya sekondari ya Yaeda chini litaangaliwa kwa utaratibu mzuri zaidi baada ya kuwasiliana na Mh.Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Dkt.Chelestino Simbalimile Mofuga  ili tuweze kumaliza bweni hilo kwani taarifa walizozipata awali hadi kupelekea jengo kutokukamilika zilikuwa siyo sahihi. Pia amewahimiza wananchi kujitokeza katika siku za kusikiliza kero za wananchi kwa kila jumanne ya kila juma hapa dongobeshi ambapo anapokea na kero za kata za jirani.





Matangazo

  • Tangazo la fursa za mafunzo ya ufundi stadi awamu ya saba February 01, 2025
  • TANGAZO LA ZABUNI YA UCHIMBAJI VISIMA January 29, 2019
  • JINSI YA KUTOA/KUTUMA MALALAMIKO KWA NJIA YA MTANDO HALMSHAURI YA WILAYA YA MBULU. March 23, 2019
  • KARIBU MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU 2021 June 10, 2021
  • Tazama zote

Habari za hivi Punde

  • MBULU DC YATOA SADAKA KITUO CHA AFYA DONGOBESH.

    January 30, 2025
  • MBULU DC YAKWAMUA VIKUNDI VYA VIJANA KIUCHUMI

    February 13, 2025
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA BAJETI YA BILIONI 38.7 KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026

    February 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI LAHIMIZA WANAFUNZI WARIPOTI SHULENI

    January 31, 2025
  • Tazama zote

Picha Jongefu

MBULU DC KUKUSANYA ZAIDI YA MIL.90 KATIKA MSIMU MPYA WA UVUVI KUTOKA BWAWA LA BONDELA YAEDA CHINI
Video za Ziada

Viunganishi ya Haraka

  • Facility Financial Accounting and Reporting System(FFARS)
  • Log in PlanRep System
  • PlanRep Documents
  • FFARS USER GUIDE
  • MANYARA REGIONAL WEBSITE
  • UTUMISHI PORTAL

link tunazolandana

  • TOVUTI YA IKULU
  • MFUMO WA VIBALI YA KUSAFIRI NJE (LIVE)
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA TAMISEMI
  • BARAZA LA MTIHANI LA TAIFA TANZANIA
  • TOVUTI YA HABARI MAELEZO

Watembeleaji wa Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Uelekeo wa Ramani

Wasiliana nasi

    Mbulu district Coucil

    Anuani: P.O.BOX 74

    Simu ya mezani: +255743583078

    Simu: +255716992222

    Barua pepe: md@mbuludc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Awali
    • Kanusho
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.