• Mlalamikaji |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Mbulu District Council
Mbulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Taasisi
    • Orodha ya Wakurugenzi
  • Utawala
    • Idara
      • Idara ya utumishi na mahusiano
      • Mipango, Takwimu na Uangalizi
      • Idara ya Fedha
      • Elimu na Utamaduni
      • Afya
      • Kilimo.Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na uthibiti wa taka ngumu
      • Uvuvi na Ufugaji
      • Idara ya Ujenzi na Zimamotto
        • Moto
      • Idara ya Maji
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Goverment Communication
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Miongozo
    • Sheria
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Picha Jongefu
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
  • Miradi
    • Miradi iliyopitishwa
    • Miradi inayoendela
    • Miradi iliyokamilika
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Dinamu
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Uchumi
      • Kamati ya Ardhi
      • Kamati ya ALAT
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba za Vikao
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Sekta ya Viwanda
    • Sekta ya Kilimo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Elimu

RAIS MAGUFULI APONGEZA JIMBO LA MBULU KUPATA ASKOFU MPYA

Kurushwa hewani: August 12th, 2018

Waziri wa Katiba na Sheria profesa Palamagamba Kabudi na Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti na viongozi mbalimbali wakifuatilia misa Takatifu ya kumweka wakfu Askofu wa Jimbo la Mbulu Anthony Lagwen.

Askofu wa Jimbo la Mbulu Anthony Lagwen akiwekwa wakfu kuwa askofu wa Jimbo hilo mjini Mbulu Mkoani Manyara 

.IMG-20180812-WA0156 (1)

Askofu wa Jimbo la Mbulu Anthony Lagwen akiwa kwenye kiti chake baada ya kusimikwa kushika nafasi hiyo mjini Mbulu Mkoani Manyara jana, kushoto ni Askofu Mkuu wa Jimbo kuu katoliki la Dar es salaam mhadhama Polycap Kardinali Pengo na Askofu mwandamizi Yuda Thadeus Ruwaichi.IMG-20180812-WA0176

Waziri wa Katiba na Sheria profesa Palamagamba Kabudi akimkabidhi Askofu wa Jimbo Katoliki la Mbulu Anthony Lagwen, zawadi iliyotolewa na Rais John Pombe Joseph Magufuli baada ya Askofu huyo kusimikwa jana mjini Mbulu Mkoani Manyara.RAIS John Magufuli amewapongeza wananchi wa wilaya za Mbulu, Babati na Hanang’ mkoani Manyara na Karatu mkoani Arusha zinazounda Jimbo la Mbulu kwa kumpata askofu wa tano wa Jimbo hilo Anthony Lagwen.Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi ambaye alimwakilisha Rais Magufuli aliyasema hayo jana mjini Mbulu Mkoani Manyara, kwenye tukio la kusimikwa kwa askofu Lagwen.Waziri kabudi alisema pamoja na kuwapongeza, kanisa katoliki limekuwa msaada mkubwa kwa serikali kwa kutoa huduma ya elimu, afya na maji hasa kwa watu wa kawaida.Alisema jimbo la Mbulu linaloundwa tangu mwaka 1953 limekuwa mfano wa kuigwa katika kuhakikisha jamii ya eneo hilo inapata huduma za kiroho na kimwili.“Tunapongeza kanisa katoliki jimbo la Mbulu kwa kutoa huduma za afya ikiwemo hospitali za misheni za Dareda na Bashnet wilayani Babati,” alisema.Alipongeza jimbo hilo kumiliki kituo cha redio Habari Njema ambacho kwa namna moja au nyingine kinatoa huduma ya uinjilishaji na kuhabarisha jamii.“Kituo hicho cha redio kiendelee kusisitiza amani kwani bila uwepo wa amani hakutawezekana kufanyika chochote,” alisema.Alisema taasisi za dini kwa kiasi kikubwa zimechangia maendeleo mengi na ustawi wa jamii hivyo serikali itaendelea kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha jamii inasonga mbele.Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dar es salaam, mwadhama Policarp Kardinali Pengo alisema japokuwa askofu Lagweni ni mzaliwa wa jimbo la Mbulu lakini atakumbana na changamoto zile zile wanazokumbana nazo maaskofu ambao wanaongoza majimbo ambayo hawajazaliwa.“Mimi siwezi kuona Sumbawanga ndiyo bora zaidi kuliko sehemu ninayoongoza waumini hivyo nawe waongoze waamini kama inavyopaswa kuwaongoza,” alisema Kardinali Pengo.Rais wa baraza kuu la maaskofu wakatoliki nchini (TEC) askofu wa jimbo la Mpanda, Gervas  Nyaisonga alisema askofu Lagwen ameteuliwa na Baba mtakatifu papa Francisco wakati huu ambapo wanasherehekea jubilee ya miaka 150 ya uinjilishaji.Askofu Nyaisonga alisema askofu Lagwen baada ya kupata nafasi hiyo anapaswa kuwaangalia usoni waumini ili kuzidi kuwajenga kiroho.Mkuu wa mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti alisema serikali ya mkoa huo itashirikiana na jimbo hilo katika kufanikisha ustawi wa wananchi wa eneo hilo.Mnyeti alisema askofu Lagweni amepata daraja hilo la uaskofu ambapo ni heshima kwa wananchi wa Mbulu, Manyara na Tanzania kwa ujumla.“Japokuwa wewe umezaliwa katika jamii ya wairaqw hata ungekuwa mmeru au msukuma lakini kwa kuwa umeteuliwa kuwa askofu wa Mbulu, umepakwa mafuta kwa uwezo wa roho mtakatifu,” alisema Mnyeti.Akizungumza baada ya kusimikwa askofu Lagwen alisema anamuomba Mungu amsaidie kutimiza wajibu wake mpya wa kiroho katika kuwahudumia waamini wa eneo hilo.Askofu Lagwen alisema wanashirikiana na serikali katika kufanikisha huduma mbalimbali na miradi ya elimu, afya, maji, mazingira, habari na nyingine.Aliwashukuru wote walifanikisha tukio hilo na akawaahidi kuwa atatoa ushirikiano unaostahili kupitia nafasi yake kwa upendo na umoja watumikie.Askofu Anthony Lagwen alizaliwa  Julai 5 mwaka 1967 kwenye Kijiji cha Tlawi, wilayani Mbulu mkoani Manyara na kuanza masomo ya elimu ya msingi na masomo ya sekondari katika seminari ndogo ya Sanu, Jimbo Katoliki la Mbulu.

mamia ya wananchi waliofurika katika viwanja vya kanisa kuu la katoliki kushuhudia kuapishwa kwa askofu

baadhi ya waumini wakiongozwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Mbulu bi Anna Mbogo mwenye Kitenge.


Timu ya waandishi wa habari njema wakiendelea na kazi



Matangazo

  • Tangazo la fursa za mafunzo ya ufundi stadi awamu ya saba February 01, 2025
  • TANGAZO LA ZABUNI YA UCHIMBAJI VISIMA January 29, 2019
  • JINSI YA KUTOA/KUTUMA MALALAMIKO KWA NJIA YA MTANDO HALMSHAURI YA WILAYA YA MBULU. March 23, 2019
  • KARIBU MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU 2021 June 10, 2021
  • Tazama zote

Habari za hivi Punde

  • MBULU DC YATOA SADAKA KITUO CHA AFYA DONGOBESH.

    January 30, 2025
  • MBULU DC YAKWAMUA VIKUNDI VYA VIJANA KIUCHUMI

    February 13, 2025
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA BAJETI YA BILIONI 38.7 KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026

    February 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI LAHIMIZA WANAFUNZI WARIPOTI SHULENI

    January 31, 2025
  • Tazama zote

Picha Jongefu

MBULU DC KUKUSANYA ZAIDI YA MIL.90 KATIKA MSIMU MPYA WA UVUVI KUTOKA BWAWA LA BONDELA YAEDA CHINI
Video za Ziada

Viunganishi ya Haraka

  • Facility Financial Accounting and Reporting System(FFARS)
  • Log in PlanRep System
  • PlanRep Documents
  • FFARS USER GUIDE
  • MANYARA REGIONAL WEBSITE
  • UTUMISHI PORTAL

link tunazolandana

  • TOVUTI YA IKULU
  • MFUMO WA VIBALI YA KUSAFIRI NJE (LIVE)
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA TAMISEMI
  • BARAZA LA MTIHANI LA TAIFA TANZANIA
  • TOVUTI YA HABARI MAELEZO

Watembeleaji wa Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Uelekeo wa Ramani

Wasiliana nasi

    Mbulu district Coucil

    Anuani: P.O.BOX 74

    Simu ya mezani: +255743583078

    Simu: +255716992222

    Barua pepe: md@mbuludc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Awali
    • Kanusho
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.