Kiswahili
  • English
  • Kiswahili
    • Mlalamikaji |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Mbulu District Council
Mbulu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Taasisi
    • Orodha ya Wakurugenzi
  • Utawala
    • Idara
      • Idara ya utumishi na mahusiano
      • Mipango, Takwimu na Uangalizi
      • Idara ya Fedha
      • Elimu na Utamaduni
      • Afya
      • Kilimo.Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na uthibiti wa taka ngumu
      • Uvuvi na Ufugaji
      • Idara ya Ujenzi na Zimamotto
        • Moto
      • Idara ya Maji
    • Kitengo
      • TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Sheria
      • Goverment Communication
  • Machapisho
    • Fomu za Maombi
    • Taarifa
    • Miongozo
    • Sheria
    • Sheria ndogo za Halmashauri
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Picha Jongefu
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
  • Miradi
    • Miradi iliyopitishwa
    • Miradi inayoendela
    • Miradi iliyokamilika
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Dinamu
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Huduma za Uchumi
      • Kamati ya Ardhi
      • Kamati ya ALAT
      • Kamati ya Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Kamati ya Ukimwi
    • Ratiba za Vikao
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Sekta ya Viwanda
    • Sekta ya Kilimo
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Elimu

Rema 1000 FC yaibuka kidedea kwa kuichakaza Lambo FC mabao 5- 3 Kurugenzi Cup'18

Kurushwa hewani: May 17th, 2018

Kurugenzi CUP ’18 yazidi kutimua vumbi katika dimba la shule ya msingi Haydom Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, kwa timu ya Rema 1000 FC kwa kuigaragaza pasipo huruma timu ya Lambo FC kwa mabao 5-3.

Katika mchezo huo uliofanyika leo alasiri timu hizo zilitoana jasho, upinzani mkali, katika kulisakata kabumbu na kuonyeshana ufundi, kwenye mashindano hayo yaliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu, Hudson Kamoga.

MchezajiGodfrey Ernest wa timu ya Rema 1000 FC ya Haydom Manyara akimtokamchezaji wa timu ya Rambo FC pia ya Haydom katika mchezo wao uliofanyikaleo kwenye uwanja wa shule ya Msingi Haydom katika Mashindano ya  kombela Kurugenzi Cup 2018 yaliyoandaliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mbuluambapo timu ya Rema 1000 FC imeibuka na ushindi wa Magoli 5-3 dhindi ya Rambo FC.

Bao la kwanza la timu ya Rema 1000 FC lilitiwa kimiani na winga machachari wao Shafii Said wenye dakika ya 26 ya kipindi cha kwanza cha mchezo huo. 

Mshambuliaji hatari wa timu ya Rema 1000 FC Masudi Juma aliipatia timu yake bao la pili kwenye dakika ya 29 mara baada ya kuwachambua pasipo na huruma walinzi watatu wa timu pinzani na kupachika kimiani bao la kiufundi, hadi mapumziko timu ya Lambo haikuona nyavu ya timu pinzani. 


 Wachezajiwa timu ya Rema 100 FC ya Haydom wakishingilia  marabaada ya mchezaji Raurenc Marco kuifungia timu yake ya Rema 1000 FC golilao la tano katika mchezo huo uliokuwa mkali dakika zote za mchezo.

Kipindi cha pili timu ya Lambo FC kupitia kocha wake ilifanya mabadiliko kwa kuwatoa washambuliaji wawili na kuingiza nguvu mpya ambayo ilibadilisha sura ya mcheo na kuleta maajabu kwenye viwanja hivyo kwa kurudisha mabao mawili na kuongeza la tatu

 Kikosi cha timu ya Rema 1000 FC kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.

Katika dakika ya 53 mshambuliaji wa timu ya Lambo FC Lazaro Zebedayo, aliyeingia kipindi cha pili alirejesha matumaini kwa kupachika bao safi la kichwa baada ya kupokea krosi safi kutoka kwa kiungo mkabaji Patrick Zacharia.

Mnamo dakika ya 60 winga machachari wa timu ya Lambo FC Salvatory Zelote aliachia shuti kali umbali wa mita 23 na kutinga kimiani na kumuacha kipa ameduwaa hivyo kufunga bao la pili na kusawazisha na kuwanyanyua mashabiki kwa vifijo na nderemo katika viwanja hivyo.

 Kikosi cha timu ya Rambo FC kikiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kwa mchezo huo.

Timu ya Lambo FC iliamka usingizini baada ya kupata mabao hayo na kuishambulia kama nyuki timu ya Rema 1000 na kufanikiwa kuandika bao la tatu kupitia mshambuliaji wao machachari Lazaro Zebedayo ambaye ndiye mfungaji wa bao la kwanza.

Benchi la ufundi kupitia kocha mkuu wa timu ya Rema 1000 Jerad Ochieng alifanya mabadiliko ya haraka kwa kumtoa kiungo mmoja na washambuliaji wawili na kubadilisha sura ya mchezo kwa muda mfupi.

Baada ya mabadiliko hayo, dakika ya 79 kulitokea piga nikupige katika lango la timu ya Lambo FC na hatimaye mshambuliaji wa timu ya Rema 1000 FC Laurence Marco alizamisha nyavuni mpira uliokuwa ukiambaa pembeni mwa goli hilo.

 Wachezaji wa timu ya Rambo FC na timu ya Rema 1000 FC wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo huo kwenye uwanja wa shule yamsingi ya Haydom.

Bao la nne la timu ya Rema 1000 FC liliwekwa kimiani na nahodha wa timu hiyo Shafii Said baada ya kutokea faulu upande wa kushoto na kupiga shuti kali lililomshinda mlinda mlango, kwa mara nyingine tena dakika mbili baada ya bao la nne kutinga kimiani, mshambuliaji Lawrence Marco alihitimisha karamu ya magoli kwa kufunga bao la kichwa baada ya kupokea krosi safi kutoka kwa kiungo mshambuliaji Masudi Juma.


 Mchezaji Ngaja Junior wa timu ya Rambo FC  bukta ya bluu na Masoud Juma wa Rema 1000 FC wakizungumza na waamuzi kabla ya kuanzarasmi kwa mchezo huo uiofanyika leo kwenye uwanja wa shule ya msingiHaydom.

 Baadhi ya watoto wakigawiwa maputo kwenye benchi la ufundi la timu ya Rema 1000 FC.

 Kocha wa Rema 1000 FC Jared Ochieng akitoa maelekezo kwawachezaji wake huku mmiliki wa timu hiyo Bw.Samson Madawa Bora ambayepia ni Daktari katika Hospitali ya Haydom akimsikiliza wakati wamapumziko ya mchezo huo.

Mara baada ya mchezo kumalizika Mkurugenzi wa timu Rema 1000 Samson Madawabora hakusita kuonyesha furaha yake katika viwanja hivyo kwa kuwazawadia kila mchezaji wa timu hiyo shilingi elfu 10,000 papo hapo uwanjani.

“Timu yetu ipo vizuri kocha wetu Jerad Ochieng ameshawapa maelezo ya kutosha wachezaji wetu hivi sasa ije timu yeyote tuu sisi sawa tutawafunga tuu kwani tupo vizuri,” alisema Madawabora.

Wakizungumza mara baada ya mchezo kumalizika kocha wa timu ya Lambo FC Paulo Modest alisema kwenye mchezo kuna matokeo matatu kushinda, kushindwa na kutoka sare hivyo anakubaliana na matokeo hayo huku kocha wa timu ya Rema 1000 FC Jerad Ochieng akisema wamejiandaa ipasavyo kwa mpambano ujao.

 Bw. Phars Nyanda Afisa Tehama Teknolojia Habari na MawasilianoHalmashauri ya wilaya ya Mbulu akitoa maelezo kwa wananchi waliofikakuangalia mchezo huo kuhusu huduma ya upasuaji kwa watu walioungua kwamoto inayotolewa na daktari wa kujitolea Joost Binmerts kutoka Uholanziakishirikiana na madaktai wa Hospitali ya Haydom.

Aidha katika kuhadhimisha wiki ya Ujasiliamali,Uwajibikaji na Uzalendo tumetumia mashindano hayo kuelimisha wananchi waliofika kuangalia mchezo huo kuhusu huduma ya upasuaji kwa watu walio na Vidonda vya Makovu,Vidonda vya Moto Mdomo wa Sungura,Matatizo ya Mikono itakayotolewa kwa nusu gharama na timu ya Madaktari wakiongozwa na Dokta Joost Binmerts kutoka Uholanzi akishirikiana na Madaktari bingwa wa Hospitali ya Haydom kuanzia tarehe 04/06/2018 hadi tarehe 15/06/2018 hospitalini hapo.

 Bw.Phars Nyanda Afisa Tehama Teknolojia Habari na Mawasiliano Halmashauriya wilaya ya Mbulu akizungumza na daktari wa kujitolea Joost Binmertskutoka Uholanzi anayefanya kazi katika  Hospitali ya Haydom.

 Baadhi ya mashabiki wa mpira waliojitokeza kushuhudia mchezo huo wakifuatilia wakati ulipokuwa ukiendelea.


Baadhi ya mashabiki wakifurahiamoja ya goli lililofungwa katika mchezo huo.

Matangazo

  • Tangazo la fursa za mafunzo ya ufundi stadi awamu ya saba February 01, 2025
  • TANGAZO LA ZABUNI YA UCHIMBAJI VISIMA January 29, 2019
  • JINSI YA KUTOA/KUTUMA MALALAMIKO KWA NJIA YA MTANDO HALMSHAURI YA WILAYA YA MBULU. March 23, 2019
  • KARIBU MWENGE WA UHURU HALMASHAURI YA WILAYA YA MBULU 2021 June 10, 2021
  • Tazama zote

Habari za hivi Punde

  • MBULU DC YATOA SADAKA KITUO CHA AFYA DONGOBESH.

    January 30, 2025
  • MBULU DC YAKWAMUA VIKUNDI VYA VIJANA KIUCHUMI

    February 13, 2025
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI LAPITISHA BAJETI YA BILIONI 38.7 KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026

    February 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI LAHIMIZA WANAFUNZI WARIPOTI SHULENI

    January 31, 2025
  • Tazama zote

Picha Jongefu

MBULU DC KUKUSANYA ZAIDI YA MIL.90 KATIKA MSIMU MPYA WA UVUVI KUTOKA BWAWA LA BONDELA YAEDA CHINI
Video za Ziada

Viunganishi ya Haraka

  • Facility Financial Accounting and Reporting System(FFARS)
  • Log in PlanRep System
  • PlanRep Documents
  • FFARS USER GUIDE
  • MANYARA REGIONAL WEBSITE
  • UTUMISHI PORTAL

link tunazolandana

  • TOVUTI YA IKULU
  • MFUMO WA VIBALI YA KUSAFIRI NJE (LIVE)
  • TOVUTI YA UTUMISHI
  • TOVUTI YA TAMISEMI
  • BARAZA LA MTIHANI LA TAIFA TANZANIA
  • TOVUTI YA HABARI MAELEZO

Watembeleaji wa Kimataifa

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

free HitCounter

Uelekeo wa Ramani

Wasiliana nasi

    Mbulu district Coucil

    Anuani: P.O.BOX 74

    Simu ya mezani: +255743583078

    Simu: +255716992222

    Barua pepe: md@mbuludc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Awali
    • Kanusho
    • Maswali yanaolizwa Mara kwa Mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.