habari na Nashon
Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu wapongeza uwepo wa timu ya Madaktari Bingwa wa Rais Samia iliyoanza kutoa huduma za kibingwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu kuanzia tarehe 06/10/2025 hadi tarehe 10/10/2025
Timu hii inaongozwa na Daktari bingwa wa Watoto, Daktari bingwa wa kinamama, Daktari bingwa wa Magonjwa ya ndani, Daktari bingwa wa Upasuaji, Daktari bingwa wa Usingizi na Daktari bingwa wa kinywa na meno
Aidha, Ujio wa madaktari hawa unakwenda kuacha alama kwani kwa mara ya kwanza hospitali hii imefanya huduma za upasuaji, sambamba na hilo ujio huu umeongeza uzoefu kwa madaktari wa halmashauri.
Ujio huu umeleta faida kwa wakazi wa halmashauri hii kupitia huduma za kibingwa kwani wananufaika na huduma zinazotolewa na timu hii ya madaktari.
Huduma hii inahusisha wanufaika wa Bima ya afya pamoja na watumiaji wa malipo kwa bei rahisi sana.
Mbulu district Coucil
Anuani: P.O.BOX 74
Simu ya mezani: +255743583078
Simu: +255716992222
Barua pepe: md@mbuludc.go.tz
Copyright ©2018 Mbulu District Council . All rights reserved.